Wanajeshi wa Azam hawa hapa kuwavaa waethiopia

Saturday August 24 2019

 

By THOMAS NG'ITU

Azam Fc leo inatupa karata yake ya pili kuelekea katika mchezo wao wa marudiano dhidi ya Fasil Kenema baada ya kupoteza katika mchezo wa kwanza waliofungwa 1-0 nchini Ethiopia.
Katika mchezo huu Azam wanahitaji matokeo ya ushindi usipongua magoli mawili ili kujihakikishia wanasonga mbele.
Kikosi cha Azam katika mchezo huu kina mabadiliko baada ya wachezaji ambao walianza kwenye mchezo wa ngao ya jamii kuondolewa na kuingia wapya.
katika mchezo wa Ngao ya Jamii, Shaban Chilunda alianza lakini kwenye mchezo huu hayupo kabisa na nafasi yake ikichukuliwa na Obrey Chirwa.
Kikosi ambacho kinaanza katika mchezo huu, Razak Abarola, Nico Wadada, Bruce Kangwa, Daniel Amoah, Yakub Mohammed, Frank Domayo, Emmanuel Mvuyekure, Salum Aboubakary, Obrey Chirwa, Djodi na Idd Seleman.
Huku upande wa wachezaji akiba Mwadini Ally, Oscar Masai, Masoud Abdallah, Salmin Hoza, Donald Ngoma, Paul Peter, Idd Kipagwile.

Advertisement