Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wilder amfukuza kazi mkufunzi wake, kisa taulo

Muktasari:

Kitendo cha mkufunzi wa Deontay Wilder kurusha taulo ulingoni wakati wa pambano lake dhidi ya Tyson Fury kimemfanya kupoteza kibarua chake

Bondia Deontay Wilder amemfukuza kazi mkufunzi wake Mark Breland akikasirishwa na kitendo cha mkufunzi huyo kurusha taulo ulingoni na kumpa ushindi Tyson Fury.
Wilder amesema bado kulikuwa na raundi tano za pambano hilo na alikuwa na uwezo wa kumaliza na kumshinda mpinzani wake huyo.
Mkufunzi huyo wa Wilder ilitupa taulo katika raundi ya saba ya pambano hilo ili kumuokoa bondia huyo aliyekuwa akivuja damu mdomoni na sikioni, pia akiwa ameangushwa mara mbili awali.
Baada ya pambano hilo Wilder na mkufunzi mkuu wa timu hiyo, Jay Deas walionyesha kutokubaliana na kitendo cha mwenzao kurusha taulo ulingoni.