Seneta aagiza app ya FaceApp ichunguzwe

Muktasari:

Ni ile iliyopata umaarufu kwa kubadili sura za watu mbalimbali kuwaonyesha wakiwa vijana au wazee

Seneta mwandamizi wa jiji la New York nchini Marekani    Chuck Schumer amewataka FBI kufanya uchunguzi kuhusu mtandao wa  FaceApp ambao umekuwa ukitumika kubadili picha ya mtu kumuonyesha akiwa mzee au kijana.

Hatua ya Shumer imekuja siku moja baada ya app hiyo kutumiwa na watu maarufu duniani wakiwamo wanamichezo, wasanii na viongozi wa siasa.

Kupitia barua aliyoiweka kwenye mtandao wa Twitter Julai 18, 2019 Schumer alisema kuwa app hiyo inamilikiwa na kampuni ya Urusi ambako ndiko yalipo makao makuu ya kampuni hiyo inachukua data za maelfu ya picha zinazotokana na utumiaji na kuwapo kwa hatari ya kudukuliwa habari zao.

Ikumbukwe kuwa vyombo vya habari vya Magharibi huhusisha chochote chenye historia ya kuwa cha Urusi huwa kinahusishwa na ujasusi.

 Kufuatia barua ya Schumer kampuni ya Wireless Lab ambayo ndiyo wamiliki wa app hiyo wameshatoa ufafanuzi  ikisema ingawa makao makuu ya app hiyo ni Urusi ila servers zinazotumika katika kupokea na kutengeneza picha mpya hazipo nchini Urusi.

Kampuni hiyo imenukuliwa na BBC ikisema kuwa wanachofanya ni kukusanya picha maalumu zilizotumwa kwa ajili ya kuzihariri.