DC akanusha mawe kuporomoka mlima Kitonga

Muktasari:

  • Mkuu wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa,  Asia Abdallah amesema hakuna tatizo lolote kwenye mlima Kitonga na magari yanaendelea kupita kama kawaida.

Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa,  Asia Abdallah amewataka Watanzania kupuuza taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa kuna mawe yameporomoka katika mlima kitonga na kuziba barabara kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha.

Akizungumza na Mwananchi leo, Asia amesema mlima huo upo salama na magari yanaendelea kupita kama kawaida.

“Nimetuma watu wameenda kufanya ‘survey’ kwenye mlima huo hakuna kitu kama hicho kwa hiyo niombe tu taarifa hizi zipuuziwe.”

“Hali ni salama na magari yanaendelea kupita kama kawaida,” amesema.