Magufuli kuzindua miradi ya Sh500 bilioni Ruvuma

Friday April 05 2019
pic miradi

Dar es Salaam. Miradi itakayozinduliwa katika mkoa wa Ruvuma na Rais John Magufuli ina thamani ya Sh500 bilioni.

Hayo yamesemwa na kaimu mkuu wa mkoa huo  Godfrey Zambi alipokuwa akimkaribisha Rais Magufuli ambaye yupo kwenye ziara mkoani humo.

Zambi amesema licha ya mafanikio makubwa yaliyopatikana mkoani humo, changamoto kubwa katika wilaya ya Tunduru ni kupambana na wanyama.

 Amefafanua kuwa licha ya kushirikiana na Wizara ya Maliasili na idara zake, bado wanahitaji kuongezewa watu kwa ajili ya kutatua changamoto hiyo.

“Tembo ni baraka kwetu na wameongezeka sana, tunaomba watuongezee watu wa idara husika ili watusaidie kupambana nao, ”amesema Zambi.

 

Advertisement
Advertisement