Wiki ya uwekezaji Kagera yaanza, wawekezaji waitwa kuwekeza

Monday August 12 2019

 

By Phinias Bashaya, Mwananchi [email protected]

Bukoba. Mkuu wa Mkoa wa Kagera (RC) nchini Tanzania, Brigedia Jenerali Marco Gaguti amefungua wiki ya Kagera kwa kuwaita wawekezaji kuchangamkia fursa zilizopo.

Katika hotuba aliyoitoa leo Jumatatu Agosti 12,2019 amesema Kagera ni eneo la kimkakati kiuchumi na kuwa fursa zilizopo zinakidhi uwekezaji wa kitaifa.

Wiki ya uwekezaji Kagera inahudhuriwa na mabalozi wote  wanaowakilisha Tanzania katika nchi za Afrika Mashariki na kati ambao pia wameambatana na makundi ya wafanyabiashara kutoka katika nchi hizo.

Kwa mujibu wa ratiba mabalozi hao wataeleza fursa za masoko, huduma na bidhaa zilizopo katika nchi hizo na jinsi ya kuzifikia huku wakielezwa fursa za uwekezaji zilizopo mkoani Kagera.

Kwa mujibu wa RC Gaguti keshokutwa Jumatano Agosti 14,2019, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atafika kuzindua mwongozo wa uwekezaji wa Mkoa wa Kagera.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa habari zaidi

Advertisement

Advertisement