Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Matokeo ya uchaguzi Liberia kutangazwa siku chache zijazo

Muktasari:

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Liberia, Jerome Korkoya amesema matokeo rasmi yanatarajiwa katika kipindi cha siku chache zijazo.

Monrovia, Liberia. Shughuli ya kuhesabu kura imeanza  nchini Liberia kufuatia duru ya pili ya uchaguzi wa rais. Uchaguzi huo utaamua ni nani atakuwa Rais mpya wa Liberia kati ya mwanasoka wa zamani George Weah na Makamu wa Rais Joseph Boakai.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Liberia, Jerome Korkoya amesema matokeo rasmi yanatarajiwa katika kipindi cha siku chache zijazo.

Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 70, taifa hilo la magharibi mwa Afrika litashuhudia Serikali iliyochaguliwa kwa njia ya kidemokrasia ikikabidhi madaraka kwa nyingine.

 Duru hiyo ya pili ya uchaguzi wa rais ilicheleweshwa baada ya kesi kuwasilishwa katika mahakama ya juu kupinga kufanyika kwa kura hiyo kwa madai ya kuwepo udanganyifu wa kura katika duru ya kwanza.