Breaking News

Kisukari husababisha kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake

Friday December 27 2019

 

By LUCY JOHN BOSCO

Wanawake wengi wenye kisukari hupata tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.

Hii inaweza kuwa ni moja ya dalili ya kisukari kwa wanawake. Hali hii mara nyingi huambatana na hasira za mara wa mara.

Mbali na kisukari, baadhi ya maradhi mengine yanayochangia tatizo la mwanamke kutosha hamu ya kufanya tendo la ndoa ni saratani na matatizo ya akili.

Matumizi ya dawa huondoa hamu ya kufanya mapenzi kwa mwanamke. Mfano wa dawa hizo ni za kukabiliana na msongo wa mawazo.

Kati ya chanzo au sababu kuu ya aina ya pili ya kisukari ni mtindo wa maisha tunayoishi, matumizi ya pombe na uvutaji wa sigara pia huchangia kukosa hamu ya tendo la ndoa.

Pia, upasuaji uliofanyika katika maeneo ya maziwa au viungo vya uzazi huathiri ufanyaji kazi wa viungo hivyo.

Advertisement

Kuna matatizo ya kisaikolojia ambayo pia yanaweza kumsababisha mwanamke kupata tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa. Matatizo ya msongo wa mawazo, kuhisi kutothaminiwa au kutokubalika katika jamii, kuwa na historia mbaya katika uhusiano na historia ya kunyanyaswa kimwili au kijinsia kama kupigwa au kubakwa.

Hali hiyo huathiri kiwango cha sukari kwa mwanamke hivyo husababisha kupanda.

Kwa upande wa matibabu, hakuna dawa au matibabu ya moja kwa moja kwa wanawake wenye kisukari isipokuwa wanatakiwa kuhakikisha sukari ipo katika kiwango sahihi.

Kiwango cha sukari ni kuanzia nne hadi nane. Lakini kabla ya kula sukari lazima iwe chini ya sita na saa mbili baada ya kula sukari inatakiwa iwe chini ya nane.

Matumizi ya dawa za sukari kwa usahihi yanaweza kusaidia kudhibiti kisukari na kurekebisha ufanyaji kazi wa homoni. Pia, mwanamke mwenye tatizo ya kukosa hamu ya tendo la ndoa lazima awe na tabia ya kuongea ili kuepuka upweke, hasira na wasiwasi.

Mwandishi wa makala haya anaishi na kisukari, muelimishaji na mshauri lishe kwa wagonjwa wa kisukari.

Advertisement