Makonda aandaa mchakato wa kupima afya bure wakazi wa Dar

Thursday September 22 2016
makonda

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam

Dar es Salaam. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam imeandaa mchakato wa kupima afya bure kwa wananchi wote.

Akizungumzia mchakato huyo mkuu  wa mkoa huo, Paul Makonda amesema kuwa utaanza siku ya Jumamosi ya na Jumapili wiki hii  katika viwanja vya Mnazi Mmoja.

Upimaji huyo utafanywa na madaktari bingwa kutoka hospitali ya Muhimbili, Ocean Road, taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete, Aga Khan na hospitali zote za rufaa za mkoa wa Dar es Salaam.

Advertisement