Wateja wa Tigo kupiga simu kwa bei nafuu nchi nzima

Dar es Salaam. Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo, leo kwa mara ya imezindua kampeni ijulikanayo kama ‘Ujanja Ni’ ikiwa na lengo la kuwapa wateja thamani ya pesa zao kila wanapotumia bidhaa za Tigo. 

Kampeni hii itawapa wateja uwezo wa kupiga simu kwenda mitandao mingine kwa gharama nafuu kupitia huduma zilizoboreshwa zaidi. 

Vifurushi vyote vya sauti vinampa mteja uhuru wa kupiga simu mitandao yote kwa bei ile ile.

Huduma hii ni ya kwanza katika soko la simu na ni suluhisho kwa wateja wa Tigo kwasababu itaweza kubadili namna ambavyo watu wanatumia huduma za mawasiliano  nchini.

“Huduma hizi zinampa mteja uhuru wa kupiga simu kwenda mtandao wowote kwa gharama ileile na wateja wanaweza kununua kifurushi chochote cha dakika, intaneti au vifurushi mchanganyiko na kufurahia faida zote muhimu kwa gharama nafuu zaidi,” alisema Kaimu Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, David Umoh.

Aidha, vifurushi vyote vimeboreshwa kwa kuongezewa muda wa maongezi, SMS pamoja na intaneti.

Pia, huduma hizi zinakuja pamoja na vifurushi vya wiki na mwezi ili kumpa mteja uwezo wa kuwasiliana zaidi, kuperuzi na kupata thamani ya pesa yake katika kila matumizi anayoyafanya.

Uzinduzi wa kampeni hii unaendana na jitihada za Serikali za kuhakikisha huduma za kupiga simu kwenda mitandao yote zinakuwa nafuu.

“Kama kampuni ya kidigitali tunaamini kuwa huduma hii itasaidia kuongeza uhuru wa mawasiliano na kuwaunganisha wateja wetu na wapendwa wao bila mipaka kutoka Tigo kwenda mitandao mingine.Tunaanzisha huduma hii chini ya kampeni iitwayo ‘Ujanja ni’ ikiwa na maana kwamba ujanja ni kutumia fursa hii ya kupiga simu kwenda mitandao yote ukiwa na Tigo,” alisema Umoh

Pia huduma hii inawapa wateja uhuru zaidi kupitia vifurushi vya wiki pamoja na mwezi vya sauti na intaneti ambavyo vina thamani zaidi sokoni.Vifurushi hivi vinadumu kwa muda mrefu huku vikimpa mteja nafasi ya kuokoa pesa kwani vinapatikana kwa bei nafuu.

“Kwa mara ya kwanza, zaidi ya wateja 12 milioni hawatakuwa na wasiwasi tena pale wanapotaka kuwasiliana na watu waliopo kwenye mitandao mingine hapa nchini. Hii inadhihirisha jitihada zetu za kuwa mtandao ambao unampa mteja thamani zaidi kupitia huduma za kibunifu,” alisema Umoh.

Ili kupata huduma hii mteja wa Tigo anaweza kupiga *147*00# na kuchagua vifurushi vya wiki na vya mwezi kupitia menyu iliyorahisishwa.