Breaking News

Hali ya hatari yatangazwa Beni, DRC

Wednesday November 27 2019

 

Beni, DRC. Mamlaka nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), imetangaza hali ya hatari katika mji wa Beni.

Aidha, Jeshi la nchi hiyo limetangaza msako wa nyumba hadi nyumba kati ya saa 12 jioni hadi saa 12 mbili asubuhi.

Gavana wa Mkoa wa Kivu Kaskazini, Charly Nzazu Kasivita, alisema jana Jumanne Novemba 26, kuwa hatua hiyo imechukuliwa baada ya kikao cha usalama kilichojumuisha wajumbe wa jeshi, polisi pamoja na vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa (EU).

Alisema “hali siyo nzuri, waandamanaji wanaongoza vurugu ambazo zimesababisha mauaji na kuharibu mali, lazima tuchukue hatua,”

Aliongeza kywa hatua hiyo ni njia mbadala ya kubaini maficho ya maadui na kulinda usalama wa raia.

Hata hivyo, hatua hiyo imepingwa vikali na wakazi wa mji huo na kusema kuwa inawanyima uhuru wao wa kutembea.

Advertisement

“Katazo hili litatuathiri sana sisi wafanyabishara wa usafiri wa bodaboda kwani wateja wetu wengi hupatikana usiku katika maeneo ya migahawa pamoja na hoteli,”alisema mmoja wa madereva hao.

Naye wakili Omari Kavota kutoka Shirika la kutetea haki la CEPADHO, alisema watu wanaogopa kutoka majumbani mwao kwa kuhofia usalama wao.

Jumanne iliyopita kikundi cha waasi kutoka nchini Uganda kiliwaa watu wanane katika mji wa Beni na kusababisha raia wenye kuandamana kupinga mauaji hayo ambako walichoma moto oisi za Meya wa mji huo.

Aidha, waandamanaji hao walilalamikia vikosi vya Jeshi la Congo pamoja na vile vya kulinda amani nchini DRC Monusco kushindwa kuwapa usalama.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, mapema leo asubuhi wanafuzi wa Chuo Kikuu mjini Goma walifunga barabara na kuelekea katika kambi za MONUSCO wakishinikiza kutotenda haki na kuvitaka vikosi hivyo ambavyo vimekuwa na miaka 20 nchini humo kuondoka.

Wanafunzi hao walifunga barabara kwa kuweka matairi na kuyachoma moto kabla ya jeshi la polisi kuwatawaya.

Taarifa ya msemaji wa Monusco, Mathias Gillmann alisema mashambulio dhidi ya kambi ya walinda usalama wa EU siyo ya kuungwa mkono.

"Taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii kwamba tunahusika kushinikiza watu kufanya ghasia ni uongo na zakupotosha.”

Advertisement