Mpenda ‘selfie’ afariki dunia baada ya kulipukiwa na simu

Wednesday September 18 2019

 

By Alinda Kato, Mwananchi [email protected]

Binti ambaye ni mhasibu amefariki dunia papo hapo kwa kupigwa shoti ya umeme baada ya simu yake iliyokuwa akiichaji kuanguka ndani ya maji.

Evgenia Shulyatyeva (26), ambaye ni mpenda ‘selfie’ alifikwa na umauti akiwa bafuni nyumbani kwao katika eneo la Kirovo, Chepetsk nchini Urusi.

Taarifa ya polisi inasema kwamba Evgenia alikuwa ameegemea ‘jaquzzi’ huku akiichaji simu yake ndipo ilipoanguka na kuingia katika maji na kulipuka.

Tovuti ya The Sun inaripoti kuwa mwili wa binti huyo uligunduliwa na mama yake mzazi Vera dakika chache baada ya tukio hilo ambalo lilisababisha kutokea kwa kishindo.

Marafiki wa Evgenia walitoa rambi rambi kwa binti huyo na kumuelezeka kuwa alikuwa mkali na anayependa kupiga picha akiwa katika sehemu mbalimbali. “Ulikuwa mkali sana Pumzika salama.”

Mwingine alisema "Dada pumzika kwa amani, lala vizuri uko milele mioyoni mwetu. Nipigie kesho, sema hiyo ilikuwa ndoto tu, kwamba hii sio ukweli."

Advertisement

Kifo binti huyo kimekuja miezi tisa baada ya msichana mwingine kufariki dunia katika tukio linalofanana na hilo.

Binti huyo Irina Rybnikova 15 alikuwa bingwa wa sanaa ya kijeshi ya Urusi aliyechaguliwa katika timu ya Taifa alipatikana amekufa ndani ya maji nyumbani kwao Bratsk, Urusi Desemba 2018.

Mkuu wa idara ya radio ya Chuo Kikuu Jimbo la Irkutsk, Yury Agrafonov alisema “maji ni hatari kwa simu ambazo zinamvutano na hiyo ndio sababu kulikuwa na mzunguko mfupi wakati simu ilipoanguka ndani ya maji.

Hata hivyo, mkuu huyo alisema endapo simu hiyo ingefungwa kwa volts 220, janga hilo lisingetokea.

Kifo cha Evgenia sasa kinachunguzwa na Kamati ya Uchunguzi ya Urusi kufuatia matukio ya vifo vinavyofanana na hiyo nchini humo.

Advertisement