Orodha ya shughuli za Bunge kutolewa kwa njia ya kimtandao

Spika wa bunge, Job Ndugai akiwasili bungeni jijini Dodoma leo, kwa ajili ya kuongoza kikao cha kwanza cha mkutano wa 16 wa bunge. Picha na Ericky Boniphace

Muktasari:

Spika wa Bunge la Tanzania,  Job Ndugai amesema leo Jumanne Septemba 3, 2019 ndio siku ya mwisho kwa shughuli za Bunge kuletwa katika chombo hicho cha kutunga sheria zikiwa zimeandikwa katika makaratasi.


Dodoma. Spika wa Bunge la Tanzania,  Job Ndugai amesema leo Jumanne Septemba 3, 2019 ndio siku ya mwisho kwa shughuli za Bunge kuletwa katika chombo hicho cha kutunga sheria zikiwa zimeandikwa katika makaratasi.

Hayo yameelezwa na Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai akibainisha kuwa Bunge hilo ndio pekee linalotumia makaratasi, kwamba mabunge mengine yameshaachana na utaratibu huo.

Amewataka wabunge kuthibitisha namba zao za simu wanazozitumia katika mtandao wa WhatsApp na email kwa ajili ya kuanza kupatiwa orodha ya shughuli za Bunge kwa siku husika kwa njia ya mtandao.

“Leo ndio mwisho wa kuingia (ndani ya Bunge) na  karatasi hizi, kuanzia kesho tutaanza kutumia  mawasiliano ya mtandao,” amesema Ndugai.