Breaking News

Cardi B ajikaanga twitter

Sunday October 18 2020

 

Rapa wa kike wa Marekani mwenye matukio ya kutikisa mitandaoni, Cardi B ameposti picha ya utupu kwa bahati mbaya kwenye akaunti yake ya Twitter ambayo baadae aliifuta haraka.

Rapa huyo ambaye jina lake halisi ni Belcalis Almanzar aliposti picha hiyo mwanzoni mwa wiki hii ambayo ilikuwa ikionesha kifua chake kikiwa wazi na baadae kuifuta. Pamoja na hilo kutokea kwa bahati mbaya alisema sio tukio linalompa ‘stress’.

Card B aliandika; ‘Ngoja niwaambie, sitajutia, wala sitajiumiza kwa hiki kilichotokea. Kufanya makosa ni kawaida kwa binadamu kwahiyo hata kosa hili haliwezi kuniumiza. Nitakunywa kifungua kinywa kwa amani kisha nitaenda kujirusha bila wasiwasi.”

Tabia hii ya wasanii wakubwa wa marekani kupost picha zao za faragha kwa bahati mbaya kwenye mitandano ya kijamii si mara ya kwanza, kwani Septemba mwaka huu , muigizaji wa filamu za Captain America, Chris Evans pia alifanya kosa hilo.

Advertisement