Hatuajiri wanawake kuonyesha sura, ATCL wamjibu mbunge CCM

Friday November 8 2019

 

By Habel Chidawali na Tumaini Msowoya, Mwananchi [email protected]

Dar/Dodoma. Wakati mbunge wa Kigoma Kusini (CCM), Husna Mwilima akisema wahudumu wa ndege za ATCL hawana mvuto kwa wateja, shirika hilo limesema haliwachagui kwa ajili ya kuonyesha sura.3

“Hatuchagui wanawake kwa ajili ya kuwapeleka kuonyesha uzuri kuna vigezo lazima tuwapime uelewa. Lazima kujua wana uwezo upi wa kufuatilia mafunzo watakayopewa ili watoe huduma inayotakiwa kwa wateja wetu na si sura,” alisema Ladislaus Matindi, mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Awali jana bungeni mjini Dodoma wakati akichangia Mapendekezo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo mwaka 2020/2021, Mwilima aliwaponda wahudumu wa ATCL kuwa hawana mvuto.

Kwa Taarifa kamili usikose Gazeti la Mwananchi Novemba 8,2019

Advertisement