Lowassa: Magufuli akiongoza miaka 10 Tanzania itapiga hatua

Muktasari:

Waziri mkuu za zamani, Edward Lowassa amesema Rais wa Tanzania, John Magufuli akiongoza nchi kwa miaka 10 itapiga hatua kubwa katika maendeleo.

Mwanza. Waziri mkuu za zamani, Edward Lowassa amesema Rais wa Tanzania, John Magufuli akiongoza nchi kwa miaka 10 itapiga hatua kubwa katika maendeleo.

Magufuli aliapishwa kuwa Rais wa Tanzania Novemba 5, 2015 na hadi leo Jumatatu Desemba 9, 2019 amefikisha miaka minne na siku 34 katika uongozi.

Lowassa aliyekuwa waziri mkuu mwaka 2005 hadi 2008 ametoa kauli hiyo katika maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika yaliyofanyika mjini Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba.

"Kama Rais Magufuli akipewa nchi hii kwa miaka 10 itakuwa ya ajabu na mabadiliko makubwa mno," amesema Lowassa aliyehama CCM mwaka 2015 na kujiunga na Chadema ambako alipitishwa kugombea urais mwaka 2015 na kushika nafasi ya pili nyuma ya Rais Magufuli.

Machi Mosi, 2019 Lowassa alirejea CCM

Akizungumza katika maadhimisho hayo waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amesema,” bado tuna kazi kubwa ya kupata uhuru wa kiuchumi kuondokana na utegemezi. Kuna kazi kubwa inafanywa na Serikali lakini bado tuna kazi kubwa ya kujitegemea kiuchumi.”