VIDEO: Mama Kayai ataka kukutana uso kwa uso na Diamond

Sunday September 22 2019

Msanii maarufu wa vichekesho nchini Kenya Mary Khavere maarufu kama Mama Kayai amesema anatamani sana kukutana na Msanii wa Tanzania Diamond Plutnumz kwa kuwa ni msanii mkubwa jambo ambalo angefurahi sana.

Mama Kayai ambaye amejichukulia umaarufu nchini Kenya katika kundi la Vitimbi  ameyasema hayo katika mahojiano na MCL DIGITAL wakati wa Tamasha kubwa la JamaFest2019 linalofanyika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

Tamasha la JamaFest ni tamasha la Utamaduni la afrika mashariki ambalo linakutanisha Burudani mchanganyiko kutoka mataifa husika huku leo Jumapili Septemba 22 Msanii Diamond Plutnamz akitarajiwa kutoa burudani .

Advertisement