Mgonjwa mwingine wa virusi vya corona aripotiwa Zanzibar

Wednesday March 25 2020Waziri wa Afya, Hamad Rashid Mohammed

Waziri wa Afya, Hamad Rashid Mohammed 

Zanzibar. Waziri wa Afya, Hamad Rashid Mohammed ametangaza kuongezeka kwa mgonjwa mwingine mmoja mwenye virusi vya corona (Covid 19) na hivyo kuwa idadi ya watu wawili Zanzibar.
Hamad ameyasema hayo leo Machi 25 wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari.
Amesema mgonjwa huyo ni mwanamke na ni mke wa aliegunduliwa mwanzoni.
Hata hivyo, ameleza kuwa Serikali imetoa siku tatu kwa kufungwa safari za kwenda na kurudi Zanzibar hivyo hakuna atakayetoka wala kuingia badaa ya siku tatu kuanzia sasa.

Endelea kufuatilia Mwananchi

Advertisement