Msekwa afunguka malalamiko ya Makamba, Kinana

Muktasari:

Msekwa alisema agizo alilowapatia viongozi hao la kujibu mapigo, wamelitii na kulitekeleza na sasa suala hilo atalikabidhi ili lishughulikiwe na vikao vya viongozi wa chama hicho waliopo madarakani.


Dar es Salaam. Katibu wa baraza la ushauri la viongozi wastaafu wa CCM, Pius Msekwa amesema malalamiko yaliyowasilishwa na makatibu wakuu wawili wa zamani wa chama hicho, Yusuf Makamba na Abdulrahman Kinana atayapeleka ngazi za juu kwa hatua zaidi.

Akizungumza na Mwananchi jana, Msekwa alisema agizo alilowapatia viongozi hao la kujibu mapigo, wamelitii na kulitekeleza na sasa suala hilo atalikabidhi ili lishughulikiwe na vikao vya viongozi wa chama hicho waliopo madarakani.

Makatibu hao wa zamani walioshika nafasi hizo katika Serikali ya Awamu ya Nne kwa kufuatana, juzi walituma malalamiko hayo kwa kuzingatia katiba ya CCM, toleo ya 2017 ibara ya 122.

Katika malalamiko yao kwa baraza hilo wamedai kudhalilishwa kwa mambo ya uzushi, uongo na mtu aliyejitambulisha kuwa mwanaharakati na mtetezi wa Serikali jambo ambalo linaelekea kuhatarisha umoja, mshikamano na utulivu ndani ya chama hicho na nchi.

Kwa undani wa habari hii soma Gazeti la Mwananchi Jumanne, 16/07/2019.

Nini maoni yako kuhusu barua ya waliokuwa makatibu wakuu wa CCM kwenda kwa katibu wa baraza la ushauri la viongozi wastaafu wa chama hicho wakilalamikia tuhuma wanazopewa, mhusika kutochukuliwa hatua?