Nabii Yaspi kuendesha maombi siku 30 kuombea corona Tanzania

Wednesday March 25 2020

 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Maambukizi ya virusi vya corona (CODIV-19) ulioanza mwaka 2019 nchini China kisha kusambaa duniani tayari umesababisha vifo vya watu zaidi ya 18,000 na wagonjwa zaidi ya 400,000 katika nchi mbalimbali.
Tanzania hadi sasa idadi ya wagonjwa ni 12 iliyotangazwa na Serikali na moja ya jitihada iliyochukuliwa ni kuwaweka watu wote wanaoingia nchini kwenye maeneo yaliyotengwa kwa siku 14.
Nabii wa Kanisa la Buza Kipera, Dar es Salaam nchini Tanzania, Yaspi Paul amewataka watu kachukua hatua ya kupambana na ugonjwa huo ugonjwa ili kuepusha na kuenea zaidi.
Amesema kanisa lake limeandaa maombi ya siku 30 kwa ajili ya kuombea kuhusu corona.
Nabii Yaspi amesema maombi hayo ni maalum kwa ajili ya ugonjwa ili kuepusha ugonjwa huu usizidi kuenea kwa kasi.
Amesema Watanzania wanapaswa kuondoa hofu kuhusu ugonjwa  huo.
"Watanzania tuondoe hofu, tuache kujipa mawazo tuchape kazi ila tuhakikishe tunachukua tahadhari tu kama watu wa afya wanavyosema, naunga mkono kauli ya Rais John Magufuli," amesema Nabii Yaspi
"Maombi haya ni muhimu tuombee taifa letu, viongozi wetu ugonjwa huu usienee uishe na wanafunzi ili waweze kurudi  katika  masomo," amesema Nabii Yaspi
Amesema maombi yao ni  kuliombea Taifa la Tanzania dhidi ya maangamizi ya virusi hivyo na kupona juu ya nchi na watu wake.

Advertisement