Takukuru: Makosa ya Lugola na wenzake yameangukia kwenye uhujumu uchumi - VIDEO

Friday February 21 2020

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imesema ndani ya wiki moja kuanzia leo Ijumaa Februari 21, 2020 itatoa jalada la uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola na wenzake 17.
Imesema jalada hilo litapelekwa ofisi ya Taifa ya mashtaka kwa kuwa makosa yote yameangukia katika uhujumu uchumi, shtaka ambalo haliwezi kupelekwa mahakamani na Takukuru.

Advertisement