Wananchi wasimamisha msafara wa Waziri Kalemani, wadai umeme

Muktasari:

  • Kalemani ambaye alikuwa njiani kuelekea eneo la Lemuguru wilayani Arumeru panapojengwa kituo cha kupoza umeme cha mradi mkubwa wa usafirishaji umeme wa Singida kwenda Namanga.

Dar es Salaam. Msafara wa Waziri wa Nishati, Medard Kalemani leo Jumapili Februari 16, 2020 umesimamishwa kwa muda baada ya barabara kufungwa na wananchi wa kata ya Murongoine kata ya Olmoti Manispaa ya Arusha wakishishikiza kuletewa umeme.

Kalemani ambaye alikuwa njiani kuelekea eneo la Lemuguru wilayani Arumeru panapojengwa kituo cha kupoza umeme cha mradi mkubwa wa usafirishaji umeme wa Singida kwenda Namanga alishuka na kusikiliza wananchi hao.

Baada ya kuwasikiliza wananchi hao Kalemani alitoa maagizo kesho Februari 17 saa 4 asubuhi Tanesco kuhakikisha wanaanza maandalizi ya kuleta umeme.

Kalemani alitoa maagizo hayo kwa Meneja wa Tanesco mkoani Arusha, Herenin Mhina kufikisha umeme eneo hilo.

"Mfikishe huduma ya umeme eneo hili kwa kuanza kupeleka nguzo na vifaa vingine haraka sana" amesema Kalemani