Wanane waibuka washindi kampeni ya Ibuka kidedea na akaunti ya NBC malengo

Muktasari:

Washindi wanane wa  kampeni ‘Ibuka kidedea na akaunti ya NBC malengo’ iliyokuwa ikiendeshwa na  Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) hadharani. Kati yao wataenda mbuga ya Serengeti huku wengine wakikwea pipa kwenda kuzulu visiwa vya Sychelles.

Dar es Salaam. Jumla ya watu wanane wameshinda kampeni ya ‘ibuka kidedea na akaunti ya NBC malengo’ iliyokuwa ikiendeshwa na  Benki ya Taifa ya Biashara.

Washindi hao wamejishindia safari za kitalii na kati yao watazulu mbunge za ya wanyama  Serengeti mkoani mara huku wengine wakikwea pipa kwenda  visiwa wa Sychelles.

Watakaokwenda Serengeti ni Christopher Mgote (Nzega),

Makongoro Makongoro (Arusha), Jocelyine Rwechengura, Esther Ndunguru wote Dar es Salaam.

Timu itakayo tembelea visiwa vya Sychelles ni Wambura Wambura (Tarime) Ramadhan Saidi, Lettice Rutashobya na Sylevester Ambokile wote Dar es Salaam.

Kampeni hiyo ilizinduliwa Oktoba mwaka huu ikiwa na lengo la kuhamasisha utamaduni wa kuweka akiba kwa wateja na zawadi mbalimbali zikiwamo bodaboda zimekuwa zikitolewa kwa washindi walioingia kwenye droo maalumu inayosimamiwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.

Akizungumza katika hafla ya kuwaaga washindi hao iliyofanyika Dar es  Salaam jana, Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Elibariki Masuke amewashukuru wote waliojitokeza kushiriki kampeni hiyo .

“Ibuka kidedea imefanyika kwa mafanikio makubwa, tumeshuhudia idadi kubwa ya wateja wetu wakishiriki katika kampeni hii, lakini pia wateja wanashuhudia

kuongezeka kwa amana zao kutokana na faida za kila mwezi,” amesema

Meneja Chapa na Mawasiliano wa NBC, David Raymond amesema  matumaini ya NBC kuwa kampeni hiyo itatoa hamasa kwa Watanzania kuwa na utamaduni endelevu wa kujiwekea akiba ili kutimiza mahitaji yao ya kifedha pamoja na kuwa na uhuru wa kifedha.

Meneja Masoko wa NBC, Alina Kimaryo amefafanua kuwa ibuka kidedea pia imekuwa ikitoa zawadi kila mwezi na hadi sasa jumla ya pikipiki tano zimeshatolewa tangu mwezi Oktoba.