Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mahakama Kuu ilivyoiokoa Bonite Bottlers kupoteza mamilioni

Mahakama Kuu Masijala Ndogo wa Dar es Salaam, imeruhusu rufaa iliyokatwa na kampuni ya Bonite Bottlers Limited na kutengua hukumu ya Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni iliyokuwa imempa Salum Nunda fidia ya Sh30milioni katika mgogoro wa mkataba wa tangazo la televisheni.

Mahakama imebaini kuwa hakukuwa na mkataba halali unaoweza kutekelezwa kisheria kwa kuwa haukuwa na kipengele muhimu cha “consideration” (malipo au manufaa ya kimkataba).

Hukumu hiyo imetolewa Mei 15, 2026 na Jaji Awamu Mbagwa, aliyekuwa akisikiliza rufaa hiyo ya madai namba 1860/2025 na nakala yake kuwekwa kwenye mtandao wa Mahakama.

Mahakama Kuu ilibaini kuwa makubaliano yaliyodaiwa kuwepo kati ya pande hizo hayakuwa mkataba halali kwa mujibu wa sheria, hivyo hayakuwa na nguvu ya kutekelezwa mahakamani.

Shauri hilo lilitokana na kesi ya madai namba 26764/ 2023 iliyofunguliwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni na Salum Nunda dhidi ya Bonite Bottlers Limited.

Katika kesi ya awali, Nunda alidai kuwa kampuni hiyo iliingia naye makubaliano ya mdomo ya kushiriki katika utengenezaji wa tangazo la televisheni la bidhaa ya maji ya Kilimanjaro kwa malipo ya Sh150milioni.

Alidai kuwa licha ya kushiriki katika utengenezaji wa tangazo hilo, kampuni hiyo ilishindwa kumlipa fedha hizo kama ilivyokubalika.

Kutokana na madai hayo, aliomba mahakama iamuru alipwe fedha hizo pamoja na riba na gharama za kesi.

Hata hivyo, Bonite Bottlers Limited ilipinga madai hayo na kueleza kuwa Nunda alikuwa mfanyakazi wake aliyeshiriki katika tangazo hilo kama sehemu ya kazi zake za kawaida, na kwamba hakukuwa na makubaliano ya kulipwa Sh150 milioni.

Kupitia ushahidi wa shahidi wake ambaye ni Ofisa Mauzo wa kampuni hiyo Charles Semari, alieleza kuwa kulikuwa na makubaliano ya maandishi yaliyosainiwa Septemba 19, 2020 yaliyomruhusu Nunda kushiriki katika utayarishaji wa tangazo hilo, huku akilipwa posho ya Sh300,000.

Aidha, kampuni hiyo ilieleza kuwa mkataba wa kutengeneza tangazo ulipewa North Advertising Agency Limited kwa gharama ya Sh14milioni.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo (North Advestising Agency Limited) Aloyce  Masawe, alithibitisha kuwa kampuni yake ndiyo iliyopewa jukumu la kuandaa tangazo hilo na kwamba Nunda alishiriki kama mfanyakazi wa Bonite Bottlers Limited na hakujua kiasi gani cha fedha ambacho alilipwa katika ushiriki wake.

Katika hukumu yake ya Desemba 11, 2024, Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni ilikubaliana na madai ya Nunda kuwa kulikuwa na mkataba wa mdomo kati yake na Bonite Bottlers Limited.

Mahakama hiyo ilisema kampuni hiyo ilivunja makubaliano hayo kwa kushindwa kumlipa fedha alizodai.

Hata hivyo, mahakama hiyo ilisema Nunda alishindwa kuthibitisha madai yake ya kulipwa Sh150milioni kwa kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuonyesha kiasi hicho kilikubaliwa.

Licha ya hivyo, mahakama ilimpa fidia ya jumla ya Sh30milioni pamoja na gharama za kesi.

Uamuzi huo uliifanya Bonite Bottlers Limited kukata rufaa Mahakama Kuu, ikidai kuwa Mahakama ya Wilaya ilifanya makosa ya kisheria kwa kutoa fidia ambayo haikuombwa wala kuthibitishwa.

Katika rufaa hiyo, kupitia wakili wake kampuni hiyo iliwasilisha sababu sita za rufaa, ikiwemo madai kuwa mahakama ya chini ilishindwa kuchunguza uhalali wa makubaliano yaliyodaiwa kuwepo na pia ilishindwa kutathmini vizuri ushahidi uliowasilishwa.

Nyingine ni Hakimu alifanya makosa katika sheria kwa kutumia kanuni zisizo sahihi na kufikia uamuzi usio sahihi na usio na msingi, Hakimu alikosea kushindwa kuchunguza uhalali wa uwepo wa uhalali wa uwepo wa makubaliano hayo ya mdomo.

Nyingine ni madai wa mjibu rufaa hiyo hayakudhibitiwa kwa kiwango kinachohitajika katika kesi za madai na Hakimu alifanya makosa kwa kushindwa kutathmini ushahidi uliotolewa na mrufani wakati wa kesi na kufikia uamuzi usio sahihi.


Uamuzi Jaji

Baada ya kupitia mwenendo, sababu za rufaa na hoja za pande zote, Jaji Mbagwa amesema hoja kuu iliyopaswa kuamuliwa ilikuwa kama kweli kulikuwa na mkataba halali kati ya pande hizo mbili.

Jaji huyo amesema ushahidi wa maandishi uliowasilishwa mahakamani kupitia kielelezo D4 ulikuwa muhimu zaidi kuliko madai ya makubaliano ya mdomo yaliyotolewa na mlalamikaji.

Amesema Nunda hakupinga saini yake katika mkataba huo wa maandishi, jambo lililoonyesha kuwa alikubaliana na masharti yaliyomo kwenye nyaraka hiyo.

“Ni msimamo wa sheria kwamba ushahidi wa maandishi hauwezi kubadilishwa kwa maelezo ya mdomo,” amesema Jaji Mbagwa katika hukumu yake.