Sahara Tanzania yaongeza hifadhi ya mafuta

Wednesday April 14 2021
mafuta pc
By Mwandishi Wetu

Dar es Salaam. Kampuni ya Sahara Tanzania Limited imeongeza ujazo wa hifadhi yake ya mafuta kufikia lita milioni 72 kwa lengo la kuongeza usambazaji kwa nchi za jirani.

“Tangu operesheni zetu zilipoanza mwaka 2015, Sahara imeongeza miundombinu kutoka vituo 10 vya kupokea na matangi manne na jumla ya hifadhi yenye uwezo wa kuchukua lita milioni 36 kwenda hadi vituo vya kupokelea 20.

“Kuongeza matangi manane yenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 72, kwa lengo la kuinua uchumi wa Tanzania kuongeza upatikanaji wa petroli,” amesema Olumuyiwa Aladejana ambaye ni Meneja mkazi wa Sahara Tanzania Limited.

Pia amesema kampuni hiyo ina mradi wa upanuzi unaolenga kuongeza hifadhi ya mafuta kuwa na uwezo wa kuhifadhi gesi ya kuendeshea mitambo (AGO), spirit ya kuendeshea mitambo (PMS) na mafuta ya ndege (JET A1).

Mradi huo kwa mujibu wa Aladejana, utaifanya Sahara Tanzania kuwa moja ya vituo vikubwa vya kuhifadhi mafuta vinavyotoa fursa za ajira kwa wingi na kuinua uchumi wa nchi.

“Ni muhimu pia kujua kwamba, kituo chetu ni cha kujiendesha na tumejipanga matangi mawili ya gesi ya petroli (LPG) yenye mita za ujazo kwa lengo la kukuza teknolojia na uhakika wa nishati kwa Tanzania, Rwanda, Zambia, Malawi na Congo,” amesema.

Advertisement

Aladejana aliyekuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utendaji kazi wa Sahara Tanzania, amesema kampuni hiyo inalenga kuunga mkono Dira ya maendeleo ya 2025 kwa kuongoza katika upatikanaji wa nishati.

Dira hiyo inatoa mwongozo wa malengo ya kuifanya nchi kufikia uchumi wa kipato ikiwa na hali bora za maosha, amani, utulivu, umoja, utawala bora jamii iliyoelimika na uchumi shindani.

“Sahara imejipanga kuchangia mafanikio ya malengo hayo kupitia kwenye miradi ya nishati na miradi ya maendeleo endelevu,” amesema.

Advertisement