Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sh2.8 bilioni kutumika ujenzi soko la kisasa la ndizi Rungwe

Mwonekano  wa eneo ambalo litajengwa soko la kisasa la zao la ndizi Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya.

Muktasari:

  • Fedha hizo zimetolewa na Serikali kwa  lengo la kuboresha miundombinu rafiki ya kibiashara na kuchangia fursa za kiuchumi na mapato ya halmashauri.

Mbeya. Serikali imetoa zaidi ya Sh2.8 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya soko la kisasa la ndizi katika Kijiji cha Mpandapanda, wilayani Rungwe, Mkoa wa Mbeya.

Ujenzi huo utajumuisha jengo la baridi la kuhifadhia mazao, maegesho ya magari, migahawa, ofisi, na eneo la huduma za kifedha, lengo likiwa ni kurahisisha biashara na kuhifadhi mazao kwa usalama.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumatatu, Novemba 24, 2025, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Rungwe, Renatus Mchau amesema mradi huu utakuwa suluhisho la wakulima kuuza zao la ndizi na kulihifadhi kwa usalama.

Mkurugenzi halmashauri ya Rungwe Renatus Mchau akisaini mkataba wa kuanza  ujenzi wa Soko la kisasa la ndizi.

Mchau pia amesema kuwa Halmashauri imesaini mkataba na Kampuni ya Kagwa General Supplies Limited kutoka Mkoa wa Singida itakayolijenga soko hilo, na ujenzi unatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miaka miwili.

Ameitaka kampuni hiyo kutekeleza mradi ndani ya muda wa mkataba ili wananchi waweze kufurahia uwekezaji wa Serikali ya Awamu ya Sita.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Emmanuel Madafa, amesema mradi huo utajengwa kwa muda uliowekwa ili kuhamasisha na kuchochea shughuli za kiuchumi katika eneo hilo.

"Mradi wa soko la kisasa la ndizi utatumia kipindi cha miaka miwili, lakini niwahakikishie tunaukamilisha ndani ya muda husika na kuukabidhi rasmi," amesema  Madafa.

Kaimu Mkurugenzi  wa Kampuni ya Kagwa General Supplies Limited, Emmanuel Madafa akisaini mkataba wa  kuanza ujenzi wa mradi wa ujenzi wa soko la ndizi  katika kijiji cha Mpandapanda Wilaya ya Rungwe mkoani hapa.

Kwa upande wake mkulima wa ndizi wa Kata ya Kiwira, Atupele Mwakyusa, amesema ujio wa mradi huo utawaondolea wakulima adha ya kufanya biashara katika maeneo yasiyo salama, hususan pembezoni mwa hifadhi za miundombinu ya barabara.