Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Utaratibu mpya wa usimamizi wa huduma za fedha ndogo wazinduliwa

Gavana wa BoT, Emmanuel Tutuba

Muktasari:

  • Uzinduzi huo uliwakutanisha wadau wakuu kutoka tasnia ya ndogo ya fedha, wakiwemo Chama cha Taasisi za Fedha Ndogo Tanzania (TAMFI) na Umoja wa Taasisi za Fedha Ndogo Tanzania (TAMIU), ambao sasa watakuwa na jukumu la msingi la kudhibiti wanachama wao chini ya utaratibu huo mpya.

Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imezindua rasmi utaratibu wa usimamizi binafsi kwa Taasisi za Fedha Ndogo za Kundi la Pili (Tier II Microfinance Institutions), hatua ambayo inatajwa kuimarisha juhudi za nchi kujumuisha wananchi katika huduma za kifedha ndogo kwa weledi zaidi.

Uzinduzi huo uliwakutanisha wadau wakuu kutoka tasnia ya fedha ndogo, wakiwemo Chama cha Taasisi za Fedha Ndogo Tanzania (TAMFI) na Umoja wa Taasisi za Fedha Ndogo Tanzania (TAMIU), ambao sasa watakuwa na jukumu la msingi la kudhibiti wanachama wao chini ya utaratibu huu mpya.

Akizungumza katika hafla hiyo, Gavana wa BoT, Emmanuel Tutuba, amesisitiza umuhimu wa utaratibu huo katika kukuza maadili, kulinda wateja, uwazi na uwajibikaji ndani ya sekta. 

“Mpango huu ni sehemu ya jitihada za jumla za kuweka mazingira rafiki ya sera na taasisi kwa utoaji wa huduma za kifedha, hususan zinazolenga watu wenye kipato cha chini na wajasiriamali wadogo,” amesema.

Utaratibu huo umetokana na makubaliano ya ushirikiano yaliyosainiwa Machi 2025 kati ya BoT na vyama hivyo viwili. Kupitia mpangilio huo, TAMFI na TAMIU watakuwa na wajibu wa kufuatilia mwenendo wa wanachama, kusimamia mifumo ya kupokea na kushughulikia malalamiko, kukuza elimu ya fedha na kuhakikisha uzingatiaji wa kanuni za serikali.

Hata hivyo, BoT itaendelea kuwa na jukumu la kusimamia na kutoa leseni ili kuhakikisha malengo ya kitaifa ya ujumuishi wa fedha na maendeleo ya sekta yanatimia kwa mujibu wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha 2020–2030 na Mkakati wa Kitaifa wa Ujumuishi wa Fedha 2023–2028.

Mfumo wa Pamoja wa Usimamizi wa Taarifa (Shared Management Information System) kwa sasa uko katika hatua za uundaji ili kuboresha uwazi wa takwimu, kupunguza gharama za uendeshaji na kuongeza ufanisi wa utoaji huduma. Gavana Tutuba ameipongeza kampuni ya UBX na SCULLT kwa ushirikiano wao katika kujenga mfumo kama huo kwa vyama vya ushirika, akieleza kuwa unaweza kuwa mfano wa kuigwa na sekta kwa ujumla.

Ili mfumo huu uanze kufanya kazi, taasisi zote za fedha ndogo za daraja la pili lazima kujisajili na TAMFI au TAMIU kabla ya Desemba 2025 na zizingatie miongozo mipya ya udhibiti.

“Mfumo huu utasaidia kubadilisha fedha ndogo kuwa chombo imara cha kuwawezesha wananchi kiuchumi,” amesema Gavana Tutuba. “Tunawaomba wadau wote waheshimu kanuni za maadili na wajenge imani ya umma katika huduma zao.”

Aidha, alitoa wito wa ushirikiano endelevu kati ya Serikali, sekta binafsi na wadau wa maendeleo ili kuhakikisha utekelezaji wenye mafanikio wa mfumo huo na kuchochea ukuaji jumuishi wa uchumi nchini kote.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Gavana, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Sadat Musa ameeleza uzinduzi wa mfumo huo kuwa ni hatua ya kihistoria katika kuboresha mazingira ya udhibiti kwa taasisi za fedha ndogo, ambazo kwa sasa zinafikia takriban 2,600 kote nchini.

Amesema BoT itaendelea kusimamia maendeleo ya sekta ili kuhakikisha yanalingana na malengo ya sera za Taifa.

Amezisihi taasisi zote za fedha ndogo za Tier II kujiunga na mojawapo ya vyama hivi viwili ili kunufaika na mifumo ya msaada, miongozo ya maadili na uongozi uliopangiliwa unaotolewa chini ya mfumo huu mpya.

“Kadri sekta inavyokuwa, udhibiti wa ndani utakuwa na nafasi muhimu katika kuhakikisha mwenendo wenye uwajibikaji na udhibiti wa sekta,” alisema.

Mwenyekiti wa Bodi ya TAMFI, Devotha Minzi, alithibitisha tena dhamira yao ya kushirikiana na BoT kuhakikisha taasisi za fedha ndogo za Tier II zinapata uaminifu wa wananchi.