Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vikwazo 10 vinavyowasubiri wafanyabiashara Tanzania, Kenya

Rais wa Kenya William Ruto akiwa na Rais Samia Suluhu Hassan. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Mwaka 2022 mawaziri wa uwekezaji wa Tanzania na Kenya walitambua vikwazo 68 na kati yake 54 vilifanyiwa kabla ya vingine vinne kuondolewa Oktoba mwaka jana.

Dar es Salaam. Wakati Tanzania na Kenya zikitarajiwa kufanya jukwaa la uwekezaji na biashara kesho Jumatatu, Mei 4 jijini Dar es Salaam, wadau wa biashara wametaka zitoe suluhisho la vikwazo 10 vya biashara vilivyokuwa vimebakia.

Katika jukwaa hili linalotarajia kuwakutanisha Rais Samia Suluhu Hassan na William Ruto wa Kenya, linalenga kuchochea ukuaji na uwekezaji wa sekta binafsi katika uchumi.

Akizungumza, Mtaalamu wa uchumi na biashara, Dk Donalth Olomi amesema kuondoa vikwazo vilivyobakia ndiyo jambo linalopaswa kupewa kipaumbele kwani bado kuna tatizo la kutokuaminiana.

“Watanzania wanawaangalia hivi Wakenya na Wakenya wanawaona hivi Watanzania inaweka ugumu katika ushirikiano na inatakiwa kufanya bidii kuondoa hicho ili kuweka usawa. Tunaweza kufanikisha hili kwa kuwakutanisha wafanyabiashara pande zote kwani wakati mwingine wasiwasi unatokana na kutokujuana,” amesema.

Katika upande mwingine amesema ni wakati kwa nchi za Afrika ya Mashariki kuungana na inapotokea fursa ya uwekezaji ichukuliwe mara moja kwa kuweka tofauti pembeni ili zifaidi huku akionya kutotanguliza kodi inayoweza kukwamisha vitu.

“Tuangalie zaidi fursa kuliko vimapato vya leo kwani ndiyo inahangia kukwamisha biashara kati ya nchi na nchi. Kama tunataka kujenga Afrika Mashariki ni vyema kuangalia hata mifumo ya elimu ambayo inamuwezesha mtoto kusoma elimu yake sehemu yoyote badala ya nchi kuwa na mfumo,” amesema.

Mtaalamu wa uchumi na biashara, Profesa Haji Semboja amesema ni vyema nchi hizo zikaangalia namna ya kudumisha uhusiano zaidi kwani ndiyo zinazoongoza katika ufanyaji wa biashara ndani ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

“Nchi hizi ndiyo kubwa Afrika ya Mashariki, zikihusiana vizuri tutafanya na wengine waone urahisi wa Burundi kuwekeza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Somalia awekeze Rwanda,” amesema.

Amesema hilo litawekezekana kwa nchi hizo kuweka sheria na sera za pamoja zitakazochochea mabadiliko na kuongeza kasi ya uwekezaji wa kiuchumi ikiwamo teknolojia mbalimbali.

“Kwa sasa katika ngazi ya utendaji ndani ya nchi hizi mbili hakuna tatizo na matokeo yanaonekana namna wafanyabiashara wa Tanzania wanavyokwenda kuwekeza Kenya na wale wa Kenya wanavyokwenda kuwekeza Tanzania, hii ni hatua kubwa na inadumisha uhusiano wetu,” amesema.

Wataalamu wanasema hayo wakati wafanyabiashara wakitaka kuondolewa kwa vikwazo vinavyoweka ugumu biashara za kuvuka mipaka.

“Kusiwe na vikwazo, mtu akitaka kwenda Kenya kupeleka mzigo au Tanzania, iwe rahisi, ikiwezekana sisi ni majirani kwa sababu tunajenga uchumi wa pande zote vikwazo viondolewe kabisa ili kuchochea ukuaji wa kiuchumi,” amesema Jensen Makangalu ambaye ni mfanyabiashara wa mahindi.

Amesema kuondolewa kwa vikwazo hivyo kutaongeza kiwango cha biashara kinachofanywa kati ya Tanzania na Kenya ambacho kitakuwa na mchango chanya katika uchumi.

Ushirikiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Kenya umeendelea kuimarika, ambapo kati ya mwaka 2020 hadi 2024, biashara ya bidhaa kati ya nchi hizo ilichangia takribani asilimia 40 ya biashara yote ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Jukwaa hili la biashara linakaliwa ikiwa ni siku 214, tangu mkutano wa tisa wa kamati ya pamoja ya biashara baina ya nchi hizo kukutana jijini Dar es Salaam na kukubaliana kuondoa vikwazo vinne kati ya 14 vilivyokuwa vimebakia.

Katika mkutano huo waliondoa kikwazo cha usafirishaji wa mbegu baada ya hati ya makubaliano kusainiwa, tozo za barabara kwa kutoza Dola 10 za Marekani kwa kila kilomita 100, kuondoa masuala ya bima ya Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (Comesa) kwa kuwa haihusiani na Tanzania.

Lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha biashara kati ya Tanzania na Kenya inafanyika kwa haki, kwa kuzingatia mikataba ya Afrika Mashariki huku Kamati ya Ufundi ya Pamoja (JTC) itakayosimamia utekelezaji wa mabadiliko hayo.

Kuondolewa kwa vikwazo hivi ilikuwa ni utekelezaji wa maagizo ya maraisi hao kwa mawaziri wa uwekezaji kuhakikisha wanaondoa vikwazo 14 vya biashara baina ya nchi hizo.

Alipozungumza baada ya kikao cha ndani, Rais Samia Oktoba 10, 2022 Ikulu Dar es Salaam ikiwa ni miongoni mwa mambo waliyojadiliana kutafutiwa ufumbuzi wa haraka kwa masilahi ya pande zote mbili.

"Kazi hii ilianza na Rais Mstaafu, Uhuru Kenyata na tulikubaliana kwa kuwataka wataalamu wetu kufanyia kazi vikwazo vya biashara vilipo.

"Mawaziri hao walitambua vikwazo 68 na vilifanyiwa kazi 54 na tumewataka sasa mawaziri wetu wakutane na kufanyia kazi vikwazo hivyo ili kuwe na uhuru wa kibiashara" amesema Rais Samia.