YARA yazindua mbolea ya MiCROP

Muktasari:

Mbolea hiyo mpya imezinduliwa Jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano mkuu wa mwaka wa wasambazaji wa bidhaa za YARA.

Dar es Salaam. Mbolea ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili wakulima nchini Tanzania, mwishoni mwa wiki kampuni  ya YARA imezindua mbolea mpya inayojulikana kama Microp kwa lengo la kuwasaidia wakulima wadogo wa mahindi na mpunga  kukuza mazao yao.

Mbolea hiyo mpya imezinduliwa Jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano mkuu wa mwaka wa wasambazaji wa bidhaa za YARA.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya YARA Tanzania, Bw. Winstone Odhiambo alisema Microp ni mbolea yenye mchanganyiko wa virutubisho vya zinc na Sulphur vinavyohitajika na mazao.

“Tunajivunia kuzindua bidhaa hii mpya ya mbolea ambayo itawasaidia wakulima wadogo wa mpunga na mahindi kupata mazao Zaidi jambo ambalo litawaingizia kipato zaidi na chakula cha kutosha,” alisema.

Kwa mujibu wa Bw. Odhiambo, mbolea hiyo itazalishwa jijini Dar es Salaam katika kiwanda cha YARA kilichoko Kurasini.

“Hii ni katika kuiunga serikali mkono katika uchumi wa viwanda kwani safari hii inazalisha hapa hapa nchini,” alisema.

Alitoa wito kwa wakulima wachangamkie mbolea hii ya Microp kwa kilimo bora zaidi na kuongeza kuwa mbolea hiyo itasambazwa nchi nzima.

Katika hatua nyingine Kampuni ya YARA imefanya mkutano wa mwaka na wasambazaji wake nchi nzima ambapo pamoja na mambo mengine wamefanya tathmini ya mwaka mzima na kuweka mipango madhubuti kwa ajili yam waka ujao.

Wakati wa hafla hiyo, wasambazaji waliovuka malengo yao walitambuliwa na kutunukiwa zawadi na kampuni hiyo.

YARA ni miongoni mwa makampuni yanayoongoza Afrika katika katika taaluma ya lishe ya mimea,mamilioni ya wakulima barani Afrika wamepata mafunzo ya mbinu bora na endelevu za kuboresha uzalishaji, kuongeza mavuno na viwango na kuongeza faida.

Mbolea ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili wakulima nchini Tanzania, mwishoni mwa wiki kampuni  ya YARA imezindua mbolea mpya inayojulikana kama Microp kwa lengo la kuwasaidia wakulima wadogo wa mahindi na mpunga  kukuza mazao yao.