22 wafariki boti ikizama Bahari ya Hindi

Muktasari:

  • Takriban wahamiaji 22 wamefariki dunia kuafuatia boti waliyokua wakisafiria kuzama baharini wakati wakielekea Kisiwa cha Mayotte, nchini Ufaransa.

Madagascar.  Wahamiaji 22 wamefariki baada ya mashua iliyokuwa imebeba watu 47 kuzama katika pwani ya Madagascar wakati ikielekea Kisiwa cha Mayotte.

 Shirika la Usafiri wa Baharini la Madagascar limesema watu 23 wameokolewa huku juhudi za kuwatafuta wengine wawili zikiendelea.

Shirika hilo limesema ajali hiyo imetokea juzi Jumamosi ambapo wahamiaji hao walikuwa wamechukua mashua kwa siri kuelekea hadi Mayotte.

Wengi wa waliookolewa wamekimbia ili wasikamatwe, Shirika la Babari la Reuters lilimnukuu ofisa wa polisi akisema.