Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

25 wadakwa maandamano ya Gen-Z Kenya

Muktasari:

  • Katika maandamano hayo bunduki tano ziliibwa, vituo vinne vya Polisi vilichomwa, biashara zilivunjwa na mali ya umma kuharibiwa.

Kenya. Watu 25 wamekamatwa nchini Kenya kutokana na vurugu zilizoibuka kwenye maandamano ya Juni 25, 2025 ya vijana maarufu Gen-Z yaliyofayika kwa lengo la kukumbuka wenzao waliouawa mwaka jana.

Katika maandamano hayo ya Jumatano iliyopita vifo, vurugu, uporaji ni miongoni mwa mambo yaliyotokea katika majiji ya Nairobi, Mombasa na miji mingine dhumuni ikiwa ni kuadhimisha mwaka mmoja tangu Gen-Z wenzao kuuawa kwenye maandamnao yaliyofanyika mwaka 2024.

Kwa mujibu wa vyombo vya nchini humo, takribani watu 60 waliuawa mwaka jana na vikosi vya usalama katika wiki za maandamano ya kupinga ongezeko la ushuru na hali mbaya ya kiuchumi kwa vijana wa Kenya pamoja na kupinga Muswada wa Sheria ya Fedha wa 2024.

 Awali, Gen-Z walipanga kufanya maandamano ya maadhimisho ambayo awali asubuhi yalikuwa ya amani ingawa muda ulivyozidi kwenda vurugu zikaibuka ndipo hekaheka ilipoanza ikiwemo mabomu kurindima huku watu 16 wakiuawa.

Polisi nchini humo imetangaza kuwakamata watu 25 wanaoshukiwa kuharibu magari ya Serikali, mahakama na biashara.

Maofisa wa idara ya upelelezi waliwakamata washukiwa hao wanaodhaniwa kuhusika na vitendo vya vurugu vilivyoshuhudiwa wakati wa maandamano hayo  Kikuyu na Kiambu.

Watuhumiwa hao wanadawa kuchoma Mahakama ya Kikuyu, ofisi za kaunti ndogo ya Kikuyu, na mali kadhaa zinazomilikiwa na serikali, yakiwemo magari na matrekta.

Idara ya Upelelezi ilichukua hatua haraka kuchunguza ghasia hizo. Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa Facebook, shirika hilo lilitangaza kuwa watuhumiwa 25 wamekamatwa na kufikishwa mahakamani kuhusiana na ghasia hizo.

"Kukabiliana na ghasia hizo, wapelelezi walianzisha uchunguzi ili kubaini na kuwakamata wahusika. Kutokana na hayo, watuhumiwa 25 wamekamatwa na kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkuu katika Mahakama ya Ruiru," DCI ilisema.

Maofisa wa upelelezi walifanikiwa kupata agizo la kuwekwa kizuizini kwa siku 14 kuwazuilia washukiwa hao huku wakiendelea kukusanya maelezo kuhusu uharibifu huo.

Hata hivyo baada ya maandamano maofisa walikamata na kurejesha baadhi ya mali zilizokuwa zimeibwa.

"Aidha, madirisha mawili ya chuma, mlango wa chuma na tanki la maji, vyote vilivyoibwa kutoka kwa ofisi za serikali ya kaunti wakati wa maandamano, vilipatikana msituni katika maeneo ya Mai-ii-hii na Kabete," akaongeza DCI.

Shirika hilo lilibainisha kuwa uchunguzi unaendelea na wanaendelea kufuatilia zaidi ili kuwabaini wengine waliohusika katika tukio hilo. DCI pia ilitoa wito kwa umma kudumisha amani wakati wa maandamano na kuonya kuwa vitendo visivyo halali havitavumiliwa.

"Jeshi la Kitaifa la Polisi linawataka wananchi kujizuia na kuepuka kujihusisha na tabia mbaya wakati wa maandamano, kwani vitendo hivyo vitachukuliwa kwa nguvu zote za sheria," iliongeza taarifa hiyo.

Waziri wa Mambo ya Ndani Kipchumba Murkomen amelaani ghasia na uharibifu  wakati wa maandamano. Akiwa amezuru Wilaya ya Kati ya Biashara ya Nairobi, Murkomen amesema wafanyabiashara wamepata hasara, huku biashara zikiharibiwa.