Azimio wamtumia taarifa IGP Kenya kuomba ulinzi maandano ya Machi 27

Mkuu wa Jeshi la Polisi la nchi hiyo (IGP), Japhet Koome

Muktasari:

  • Azimio la Umoja, Kenya wamuandikia barua IGP, Japhet Koome wakimjulisha nia ya kufanya maandamano yatakayofanyika  ijayo Machi 27 na Machi 30.

Dar es Salaam. Muungano wa Azimo la Umoja nchini, Kenya umemwandikia barua Mkuu wa Jeshi la Polisi la nchi hiyo (IGP), Japhet Koome kumtaarifu kuhusu kufanya maandamano na maombi ya Kitaifa.

Barua hiyo iliyosainiwa na mwenyekiti wa halmashauri kuu ya Azimio la Umoja, Dk Wycliffe Oparanya imeandikwa leo Jumatano Machi 22, 2023 kwenda kwa mkuu huyo wa polisi.

Hatua hiyo, imekuja baada ya kupita siku tatu kwa Azimio la Umoja kupitia kiongozi wao, Raila Odinga kuongoza maandamano yaliyofanyika katika miji mbalimbali ya Kenya wakishinikiza Serikali ya Dk William Ruto kuleta unafuu wa maisha na hali bora ya uchumi kwa Wakenya.

Katika maandamano hayo, mwanafunzi wa Chuo Kikuu nchini Kenya alifariki dunia huku maofisa sita wa polisi wakijeruhiwa kwenye purukushani hizo.


Lakini Dk Oparanya kupitia barua hiyo, amemtaarifu Koome nia yao ya kufanya maandamano kuanzia Machi 27 na Machi 30 katika kaunti 47 za Kenya. Amesema watakuwa wakifanya hivyo kila Jumatatu na Alhamisi zitakazofuata.

“Tunakusudia kuwasilisha maombi kwa makamanda wa kaunti; makamanda wa kaunti ndogo na ofisi zingine zote za majimbo yote nchini kama sehemu ya maandamano. Hakuna mashaka, hili sio ombi la kibali kwa sababu hakuna kinachohitajika chini ya Kifungu cha 37.

“Tunakuomba ushirikiano kwa kutoa polisi watakaolinda usalama wakati wote wa maandamano. Kwa taarifa hii tunaomba utupatie ulinzi,”amesema Dk Oparanya.

Dk Oparanya ameongeza kuwa sema, “Kwa taarifa hii tutaruhusu polisi wenye sare, watakaovalia kiraia tutawachukulia kama wanataka kuhatarisha usalama na amani kwa raia au wametumwa kuleta vurugu.