Marekani yashambulia kundi la Taliban

Wapiganaji wa Taliban walikua wakisherehekea mkataba wa Marekani mapema wiki hii.AFP

Kabul, Afghanistan. Ndege za Marekani zimefanya mashambulizi ya angani dhidi ya kundi la Taliban.

Shambulizi hilo limekuja siku moja baada ya pande hizo kutia saini makubaliano ya amani mwishoni mwa wiki iliyopita.

Pande hizo zilikutana Jumatano iliyopita kufuatia mauaji ya askari 32 wa jeshi la Afghanistan kutokana na hujuma zilizofanywa na Taliban kwenye majimbo matatu.

Taarifa ya jeshi la Marekani ilisema kuwa  mashambulizi yaliyofanywa na ndege za Marekani yalilenga kujihami dhidi ya Taliban baada ya wapiganaji hao kuyashambulia majeshi ya Afghanistan kwenye jimbo la Helmand lililopo Kusini mwa nchi hiyo.

Kwa upande wake Taliban ilisema kundi hilo litaendelea kupigana mpaka hapo makubaliano ya ndani yatakapofanikiwa.

Katika makubaliano hayo Marekani na Taliban walikubalina kuondoa majeshi ya  nje yataondoka kutoka Afghanistan katika kipindi cha miezi 14. Makubaliano hayo pia yameweka msingi wa mazungumzo ya ndani kati ya Taliban na serikali ya Afghanistan.