Miili ya waliofunga wakiamini kwenda mbinguni yafikia 89

Muktasari:

  • Dunia inaendelea kushangazwa na miili inayoendelea kufukuliwa katika Kaunti ya Kilifi nchini Kenya ambayo inadaiwa ni ya waumini waliofariki dunia kwa kufunga wakiamini wangeenda mbinguni baada ya kifo chao.

Kenya. Idadi ya miili ya waumini waliofariki dunia kwa kufunga imefikia 89 katika shughuli za ufukuaji wa makaburi zinazoendelea katika Kijiji cha Shakahola, Kaunti ya Kilifi nchini Kenya.

Polisi wameendelea oparesheni ya kufukua makaburi hayo yanayodhaniwa kuzikwa waumini wa waumini wa Kanisa la Good News International walioshawishiwackufunga wakiamini wakifa wataenda mbinguni.

Ofisa wa Upelelezi wa mauaji nchini humo amesema wanaendelea makaburi ya halaiki kwenye kipande cha ardhi cha ekari 800 ambacho ni mali ya kiongozi wa Kanisa la la Good News International, Paul Mackenzie anayedaiwa kushawishi waumini hao.

Mchungaji Mackenzie alikamatwa Aprili 14, mwaka kufuatia taarifa iliyodokeza kuwepo kwa makaburi yenye miili ya baadhi ya wafuasi wake.

Mackenize alifikishwa mbele ya Hakimu Mkuu Mfawidhi wa Malindi, Elizabeth Usui na hakutakiwa kujibu shitaka lolote, huku upande wa mashtaka ukitaka siku 30 zaidi za kumshikilia watakapokamilisha upelelezi.

Alifikishwa mahakamani pamoja na watu wengine 13 katika kesi itakayotajwa Mei 2, mwaka huu.


Imeandaliwa na Pelagia Daniel.