Rais wa Senegal amfukuza kazi Waziri wa Afya

Muktasari:

  • Nafasi ya Sarr itachukuliwa na Marie Khemesse Ngom Ndiaye, mkurugenzi mkuu waWizara ya Afya.

Dakar. Rais wa Senegal, Macky Sall amemfukuza kazi Waziri wa Afya wa nchi hiyo, Abdoulaye Diouf Zarr baada ya watoto wachanga 11 kuuawa kwa moto katika chumba cha hospitali cha watoto wachanga.


Meya wa mji wa Tivaouane, Demba Diop amesema moto huo ulisababishwa na hitilafu ya umeme na ulisambaa kwa haraka kuua watoto hao wachanga.


Rais Macky Sall ametoa taarifa ya msiba huo kwenye Twitter na kutangaza siku tatu za maambolezo ya kitaifa.


Nafasi ya Sarr itachukuliwa na Marie Khemesse Ngom Ndiaye, mkurugenzi mkuu waWizara ya Afya.