Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais wa Somalia awataka kuwafichua Al-Shabaab

Muktasari:

Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud ametoa wito kwa watu wa mbalimbali kusaidia kuwaondoa wanachama wa kundi la wanajihadi la Al-Shabaab aliowataja kuwa ‘kunguni’.

Dar es Salaam. Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud ametoa wito kwa watu wa mbalimbali kusaidia kuwaondoa wanachama wa kundi la wanajihadi la Al-Shabaab aliowataja kuwa ‘kunguni’.

Kwa mujibu wa kituo cha habari ‘AFP’ wameeleza kwamba Mohamud alikuwa akihutubia umati wa watu katika mkutano ulioandaliwa na serikali dhidi ya wanamgambo hao wenye kufungamana na Al-Qaeda uliofanyika katika uwanja wa michezo katika mji mkuu Mogadishu ukiwa chini ya ulinzi mkali.

" Waasi wapo miongoni mwenu... kwa hiyo watoeni nje. Wako kwenye nyumba zenu, ni majirani zenu, kwenye magari yanayopita kwenu," amesema.

"Nataka tujitolee kuwaondoa, ni kama kunguni ndani ya nguo zetu," aliongeza Rais huyo, huku waandamanaji wakipeperusha bendera na mabango yenye ujumbe dhidi ya Al-Shabaab.

Al-Shabaab imekuwa ikiendesha uasi wa umwagaji damu dhidi ya serikali kuu inayoungwa mkono kimataifa kwa miaka 15.

Kundi hilo limekuwa likifanya mashambulizi nchini Somalia na nchi jirani.

"Watu wamechoshwa na mauaji na kila aina ya uovu na sasa wanawaambia Al-Shabaab, 'Inatosha'," amesema Rais Mohamud.

Rais huyo alitangaza vita dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu muda mfupi baada ya kuingia madarakani Mei mwaka jana.

Katika miezi ya hivi karibuni, jeshi na wanamgambo wa koo wameteka tena maeneo mengi katikati mwa nchi katika operesheni iliyoungwa mkono na mashambulizi ya anga ya Marekani na kikosi cha Umoja wa Afrika.

Lakini waasi hao mara kwa mara wamelipiza kisasi kwa mashambulizi ya umwagaji damu, wakisisitiza uwezo wao wa kushambulia katikati ya miji ya Somalia na vituo vya kijeshi.

Ingawa walilazimishwa kuondoka Mogadishu na vituo vingine vya mijini zaidi ya muongo mmoja uliopita, Al-Shabaab bado wamejikita katika maeneo ya vijijini, katikati na kusini mwa Somalia.