Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sita wafariki harusini, vilio vyatawala

Wananchi wa Kihunguro, Ruiru katika Kaunti ya Kiambu nchini Kenya wakiwa katika kisima ambacho watu sita walipoteza maisha baada ya kutumbukia ndani yake.

Muktasari:

  • Vilio vimetawala katika tukio la harusi baada ya watu sita kufariki walipokuwa wakihudhuria tukio hilo kufuatia kutumbukia katika kisima kilichokuwa eneo hilo baada ya kukanyaga juu yake.

Kenya. Watu sita wamefariki walipokuwa wakihudhuria tukio la harusi baada ya kutumbukia katika kisima kilichokuwa eneo hilo baada ya kukanyaga juu yake.

Tukio hilo limetokea leo Jumamosi asubuhi huko Kihunguro, Ruiru, kaunti ya Kiambu nchini Kenya baada ya kisima kutumbukia baada ya kuzidiwa na uzito wa watu waliokuwa wakiimba na kucheza juu ya kisima hicho.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Star, Polisi wamesema kundi hilo lilikuwa limefika katika makazi hayo kwa ajili ya sherehe ya harusi ambapo walikuwa wamesimama kwenye kisima cha zege.

Wamesema waathiriwa sita wakiwemo watoto walifariki baada ya mfuniko wa kisima kuporomoka na kuwazamisha huku wengine 17 wakijeruhiwa.

Kulingana na polisi, kutokana na uzito wa kundi hilo, kifuniko cha zege cha kisima kilianguka na kuwazamisha.

Mtoto mmoja alifariki papo hapo huku kundi jingine likiokolewa na kukimbizwa hospitalini.

Polisi walisema wengine watano walithibitishwa kufariki walipofika katika hospitali moja huko Ruiru.

Kikosi cha zima moto kutoka Kiambu kilikimbia kuokoa kundi hilo lililokuwa limenasa kwenye tanki la maji la chini ya ardhi.

Gavana wa Kiambu Kimani Wamatangi alithibitisha tukio hilo.

“Wengi wao wameokolewa kupitia juhudi za serikali ya Kaunti ya kikosi cha zima moto cha Kiambu na wanajamii. Kazi ya uokoaji inaendelea. Tunasikitika kwa familia zilizoathiriwa na tunawatakia waathiriwa ahueni ya haraka,” amesema Wamatangi.

Tukio hilo lilisababisha kuahirishwa kwa harusi huku polisi wakiendelea na uchunguzi.