Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watoto wanne wakutwa hai wiki tano baada ya kuanguka ndege

Wanajeshi wa Colombia wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uokoaji wa watoto walionusurika katika ndege aina ya Cessna 206 iliyoanguka Mei 1 katika misitu ya Caqueta, katika mpaka ya Caqueta na Guaviare.

Muktasari:

  • Katika hali isiyo ya kawaida, watoto wanne wa familia moja wamenusurika kifo katika ajali ya ndege iliyotokea wiki tano baada ya ajali hiyo nchini Colombia.

Colombia. Watoto wanne nchini Colombia wamepatikana wakiwa hai kusini mwa nchi hiyo jana Ijumaa ikiwa ni wiki tano baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kuanguka katika msitu mkubwa, Rais wa Colombia Gustavo Petro amesema.

Watoto hao waliokolewa na wanajeshi karibu na mpaka kati ya majimbo ya Caqueta ya Colombia na Guaviare, karibu na mahali ambapo ndege ndogo waliyokuwa wakisafiria kuanguka.

Ndege hiyo aina ya Cessna 206  ilikuwa imebeba watu saba ikiwa njiani kati ya Araracuara, katika jimbo la Amazonas, na San Jose del Guaviare, mji wa jimbo la Guaviare ilipata ajali muda mchache baada ya taarifa ya hitilafu ya injini mapema Mei 1.

Watu wazima watatu akiwemo rubani na mama wa watoto hao Magdalena Mucutuy walifariki dunia kutokana na ajali hiyo na miili yao kupatikana ndani ya ndege hiyo. Ndugu hao wanne, wenye umri wa miaka 13, 9, 4, pamoja na mtoto mchanga mwenye umri wa miezi 12 sasa, walinusurika katika ajali hiyo.

Narcizo Mucutuy, babu wa wasichana hao watatu na mvulana mmoja, aliwaambia wanahabari kuwa alifurahishwa na habari za kuokolewa kwao.

"Kama babu kwa wajukuu zangu waliotoweka kwenye msitu wa Yari, kwa sasa nina furaha kubwa," alisema.

Wanajeshi wa Colombia wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuwaokoa watoto wanne walionusurika katika ndege aina ya Cessna 206 iliyoanguka Mei 1 katika Misitu ya Caqueta, katika mipaka ya Caqueta na Guaviare.