Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watu milioni 14 wanaweza kufariki baada ya USAID kupunguza misaada

Muktasari:

  • Utafiti huo umeonya kwamba athari zinaweza kuonekana katika sekta ya mapambano ya magonjwa kama VVU/Ukimwi na malaria.

Dar es Salaam. Utafiti uliochapishwa kwenye jarida la The Lancet jana Jumatatu umebaini hatua ya Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) kupunguza msaada wa kifedha inaweza kusababisha vifo zaidi ya milioni 14 duniani kote ifikapo mwaka 2030.

Utafiti huo umeonya kwamba athari zinaweza kuonekana katika sekta ya mapambano ya magonjwa kama VVU/Ukimwi na malaria na maradhi mengine ikiwemo kuhara pamoja na watoto wadogo.

Habar hiyo inachapishwa wakati Mkutano wa nne wa Kimataifa wa Ufadhili wa Maendeleo (FfD4) unaofanyika nchini Hispania ukiendelea ambapo viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Philip Mpango, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), António Guterres, Rais wa Hispania, Pedro Sánchez wamehudhuria kujadili masuala ya ufadhili wa maendeleo. 

Katika utafiti huo watafiti wamechambua taarifa za vifo kutoka nchi 133 zenye kipato cha chini na cha kati kuanzia mwaka 2001 hadi 2021 na kubaini programu za afya zilizokuwa na mkono wa USAID zimezuia takribani vifo milioni 91.8 katika miongo hiyo miwili. 

Uchambuzi wa mifumo (modelling) unapendekeza wimbi la sasa la kupunguzwa kwa fedha linaweza kufuta maendeleo hayo, na uwezekano wa kusababisha vifo vya ziada kati ya milioni 1.78 na milioni 2.5 kila mwaka kati ya 2025 na 2030.

Programu zinazoungwa mkono na USAID zilihusishwa na kupungua kwa asilimia 15 ya vifo kutokana na sababu zote, watafiti waligundua. Kwa watoto walio chini ya miaka mitano, kushuka kwa vifo kulikuwa mara mbili zaidi, yaani asilimia 32.

Ufadhili wa USAID uligunduliwa kuwa na ufanisi hasa katika kuzuia vifo vinavyoweza kuzuilika kutokana na magonjwa. Kulikuwa na kupungua kwa asilimia 65 ya vifo kutokana na VVU/Ukimwi katika nchi zilizopokea msaada wa hali ya juu ikilinganishwa na zile zenye ufadhili mdogo au zisizo na ufadhili wowote wa USAID. Vifo kutokana na malaria na magonjwa yaliyosahaulika ya kitropiki navyo vilipungua kwa nusu.

Baada ya USAID kupunguza msaada, wafadhili wengine wakuu kadhaa ikiwemo Ujerumani, Uingereza na Ufaransa walifuata kwa kutangaza mipango ya kupunguza bajeti zao za misaada ya kigeni.

"Kukosekana huku kwa ufadhili kunaweza kuleta moja ya vikwazo vikubwa zaidi kwa afya ya kimataifa katika miongo kadhaa," amesema mwandishi-mshiriki Davide Rasella wa Taasisi ya Barcelona ya Afya ya Kimataifa (ISGlobal). 

"Kuna hatari ya kusababisha mamilioni ya vifo vinavyoweza kuzuilika, hasa miongoni mwa walio hatarini zaidi, na kurudisha nyuma maendeleo katika afya na maendeleo ya kiuchumi na kijamii."ameongeza.

Ripoti hiyo inahusisha sehemu kubwa ya maisha yaliyookolewa kihistoria na kazi ya USAID juu ya VVU/Ukimwi, ikikadiria kupungua kwa karibu theluthi mbili ya vifo vinavyohusiana takribani watu milioni 25.5 katika kipindi cha utafiti. 

Programu zinazoshughulikia Malaria, magonjwa ya kuhara, magonjwa yaliyosahaulika ya kitropiki, na maambukizi ya mfumo wa chini wa upumuaji zilipewa sifa ya kuokoa maisha mengine milioni 31.

Hata hivyo, rekodi hiyo ya mafanikio iko hatarini. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio aliliambia Bunge Machi mwaka huu kwamba asilimia 83 ya miradi ya USAID ingesitishwa, huku iliyobaki ikiunganishwa na Wizara ya Mambo ya Nje. 

Aidha, Waziri wa Afya wa Marekani Robert F. Kennedy Jr. alitangaza wiki iliyopita kusitishwa kwa mchango wa Washington wa dola milioni 300 kila mwaka kwa Gavi, shirika la kimataifa la chanjo ambalo kihistoria lilipitishwa kupitia USAID.

Shirika la Habari la Reuters limesema kati ya makadirio hayo ya watu zaidi ya milioni 14  walio, theluthi moja yao wakiwa watoto wadogo, wanaweza kufa kutokana na kuvunjwa kwa misaada ya kimataifa ya Marekani na utawala wa Trump.

Shirika la USAID lilikuwa likitoa zaidi ya asilimia 40 ya fedha za msaada wa kibinadamu duniani hadi Donald Trump aliporejea Ikulu ya White House Januari mwaka huu.
             
Wiki mbili baadaye, mshauri wake wa karibu wa wakati huo  na tajiri mkubwa zaidi duniani  Elon Musk alijigamba kwa kile alichokisema kuwa ameliweka shirika hilo ‘kupitia mashine ya kusagia kuni