‘Kapu la wana’ la SBL latema washindi saba

Muktasari:
- Baada ya droo ya kwanza kufanyika siku kadhaa zilizopita, wiki hii Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) imechezesha droo yake ya pili kupitia kampeni ya bia yake ya Pilsner lager na kuibuka na washindi waliojipatia zawadi mbalimbali zikiwamo pikipiki.
Dar es Salaam. Serengeti Breweries Limited (SBL) kupitia kampeni ya bia yake ya Pilsner lager iliyopewa jina la ‘Kapu la wana’, imekabidhi zawadi ya pikipiki na zawadi nyingine kwa washindi saba katika droo yake ya pili.
Droo hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki imeibuka na washindi kutoka mikoa ya Kilimanjaro, Mwanza na Mbeya.
Katika droo hiyo, washindi watatu waliondoka na simu za mkononi, watatu wengine walijipatia seti za televisheni na mshindi mmoja alizawadiwa pikipiki.
Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika kwa wakati mmoja katika kanda ya Ziwa, Kaskazini na Kusini ambako kampeni ya ‘Kapu la Wana’ inahusika.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa zawadi yake mkoani Kilimanjaro, mshindi wa pikipiki, Lazaro Kileo alisema anafuraha kuibuka na ushindi huku akisema kampeni hiyo imekuwa msaada kwake.
“Kampeni hii inasaidia kuinua uchumi watu, tunapotunukiwa zawadi kama pikipiki ambazo tunaweza kuzitumia kujiongezea kipato, haya ni maendeleo makubwa na inatuondolea umaskini,” alisema Kileo.
Washindi wengine watatu wa kampeni hiyo ya 'Kapu la Wana' walioondoka na simu za kisasa ni pamoja na Lucy Faustine (Korogwe), HeinstenTumaini (Kagera) na George Gerald (Katavi).
Wengine watatu waliojishindia runinga za kisasa ni pamoja na Abdul Msafiri (Arusha), Salumu, Nyanga (Simiyu) na Happy Venance (Iringa).
Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja Mauzo wa SBL Mkoa wa Kilimanjaro, Abel Mushi aliwapongeza washindi hao akisema dhumuni la kampeni ya ‘Kapu la Wana’ ni kuwajengea uwezo watumiaji wanaofanya kazi kwa bidii kwa kuwazawadia zawadi mbalimbali pindi watakaposhiriki katika kampeni hiyo.
“Tunawathamini wateja wetu na hii ndiyo njia yetu ya kuwatunza kwa kupenda na kuunga mkono chapa yetu, hii ni mara ya pili tunaendesha kampeni hii na kupitia kampeni hii, tunataka kuwapa wateja wetu fursa ya kuinua maisha yao kwa njia moja au nyingine. kwa mfano mshindi wa pikipiki anaweza kuamua kuitumia ili kusaidia kuongeza mapato yake na kwa upande mwingine, washindi wa runinga mahiri na simu mahiri zawadi zao zitaendeleza ustawi wao wa kijamii.”
Alitoa wito kwa watumiaji katika kanda za Ziwa, Kusini na Kaskazini kuendelea kushiriki katika kampeni na kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali katika kampeni hiyo ya muda wa wiki 8 ambayo ilizinduliwa Februari 2, mwaka huu. Zawadi hizo ni pamoja na runinga mahiri, simu mahiri, pikipiki na zawadi kubwa ya gari ambalo ni jipya kabisa.
SBL imewekeza jumla ya Sh36 milioni katika kampeni ya kuwapata washindi 22 hadi mwisho wa kampeni.