Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Kibakuli’ afungwa miaka 30 jela baada ya kukiri kulawitiwa kwa kujitakia

Muktasari:

  • Mwanaume ahukumuwa miaka 30 jela baada ya kukiri kuingiliwa kinyume na maumbile.

Mbeya. Mahakama ya Wilaya ya Kyela  mkoani Mbeya imemhukumu kutumikia kifungo cha miaka 30 jela Claud Mwinuka (22)  maarufu  kama ‘Kibakuli’ baada ya kukiri kosa la kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile.

Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Paul Barnabas jana Alhamisi 6, 2023 baada ya mtuhumiwa kufikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo na kusomewa mashtaka yanayomkabili.

Amesema Mahakama imemtia hatiani mtuhumiwa baada ya kukiri kosa  la  kuruhusu kuingilia kinyume na maumbile na wanaume, huku akijua ni kosa la kifungu cha 154 kifungu kidogo cha kwanza (C )cha sheria ya kanuni ya adhabu kama ilivyorekebishwa mwaka 2022.

Hakimu Barnabas amesena wametoa  hukumu kwa mtuhumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela ili iwe fundisho kwa watu wengine wanajihusisha na tabia hiyo.

“Upande wa Jamhuri umetoa adhabu hiyo kwa mujibu wa sheria ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia za kuingiliwa kinyume cha maumbile kwa kujitambua,”amesema.

Awali inadaiwa mtuhumiwa alisambaza picha za video kwenye mitandao ya kijamii

 zikimuonyesha akiwa amevalia mavazi ya kike huku akitembea usiku wa manane ambapo alikamatwa na  sungusungu waliokuwa doria na kufikisha katika vyombo vya dola.

Mkazi wa Mikoroshini wilayani humo, Anna Sanga ameiomba jamii kuwafichua wanaume wenye tabia hizo chafu  ili sheria ichukue mkondo wake kwani wamekuwa wachafua tamaduni za Kitanzania.