#Live: Kuapishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Bashiru Ally

#Live: Kuapishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dk Bashiru Ally

Muktasari:

  • Rais John Magufuli amemteua katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally  kuwa katibu mkuu kiongozi kuchukua nafasi ya Balozi John Kijazi aliyefariki dunia Februari 17, 2021.

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemteua katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally  kuwa katibu mkuu kiongozi kuchukua nafasi ya Balozi John Kijazi aliyefariki dunia Februari 17, 2021.

Taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa mawasiliano ya rais Ikulu, Gerson Msigwa leo Ijumaa Februari 26, 2021 inaeleza kuwa kiongozi mkuu huyo wa nchi pia amemteua Dk Bashiru kuwa Balozi.

“Uteuzi wa Dk Bashiru unaanza leo Februari 26 na ataapishwa kesho saa 3:00 asubuhi jijini Dar es Salaam, “ inaeleza taarifa hiyo.

Mei, 2018 Dk Bashiru aliteuliwa kuwa katibu mkuu wa CCM akichukua nafasi ya Abdulrahman Kinana.

Uteuzi huo ulifanywa na Rais Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho na kuthibitishwa na wajumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho tawala nchini Tanzania ikiwa ni siku kadhaa tangu msomi huyo aongoze mchakato wa kuhakiki mali za CCM.

Kabla ya kuteuliwa kuwa katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru alikuwa mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) katika idara ya sayansi ya siasa na alikuwa akiongoza kurugenzi ya mijadala na makongamano.