Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Moto wateketeza mali za wapangaji, Sh3.4 milioni

Moja ya chumba ambacho kimeteketea kwa moto l

Muktasari:

  • Vyumba hivyo vitatu vimeteketea kwa moto leo huku ikiziacha kaya tatu bila makazi.

Moshi. Moto ambao chanzo chake hakijajulikana umeteketeza vyumba vitatu vya wapangaji katika Mtaa wa Wailesi, Kata ya Soweto, Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro wakati wakijiandaa kupika chakula cha mchana kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya 2025.

Vyumba hivyo vitatu vimeteketea kwa moto leo , Januari Mosi, 2025  ambapo kaya tatu kwa sasa hazina mahali pa kuishi baada ya moto huo  kuteketeza samani na mali zote ikiwemo fedha taslim Sh3.4 milioni.

Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoani Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi amesema chanzo cha moto huo bado hakijafahamika na wanaendelea kuchunguza tukio hilo.

Amesema pamoja na vyumba hivyo kuteketea kwa moto fedha taslimu Sh3.4 milioni zilizokuwemo ndani kwenye vyumba hivyo zimeteketea kwa moto.

"Leo saa 7:19 mchana tulipokea taarifa ya kuwepo kwa tukio la moto kwenye nyumba ya makazi, tuliondoka kituoni saa 7:20 tulikuta moto tayari umeenea katika vyumba vitatu, shughuli ya uzimaji moto iliendelea na tulifanikiwa kudhibiti moto usienee maeneo mengine,"amesema Kamanda Mkomagi

Kamanda Mkomagi amesema moto huo haujasababisha madhara ya kibinadamu na walifanikiwa kuokoa baadhi ya mali zilizokuwemo ndani na nyingine ziliteketea kwa moto.


Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa eneo hilo, Diwani wa kata ya Soweto,  Charles Mbando amesema tukio hilo limewafanya baadhi ya watu kuanza mwaka 2025  vibaya kwa kuwa wamepoteza mali zilizokuwemo ndani ya vyumba hivyo.

"Siku ya kwanza ya mwaka 2025 ni kama tumeianza vibaya, vyumba vitatu vyote vya kaya tatu kuteketea kwa moto inahuzunisha, lakini tunalishukuru Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kufika mapema katika eneo hili na kudhibiti moto usienee kwenye maeneo mengine,"amesema Diwani Mbando

Ameongeza kuwa watakaa kikao kuona namna ya kuzisaidia familia hizo kwa kuwa zimeachwa bila chochote, huku akisema watapitisha daftari la mchango kwenye mtaa huo ili kuzisaidia familia hizo.