Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

RC Kagaiga aagiza kuharakisha ujenzi Ofisi ya Halmashauri Moshi

RC Kagaiga aagiza kuharakisha ujenzi Ofisi ya Halmashauri Moshi

Muktasari:

  • Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Stephen Kagaigai amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi ,Kastory Msigala kuharakisha  ujenzi wa ofisi za makao makuu ya halmashauri hiyo zinazojengwa eneo la Sango.

  


Moshi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Stephen Kagaigai amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi ,Kastory Msigala kuharakisha  ujenzi wa ofisi za makao makuu ya halmashauri hiyo zinazojengwa eneo la Sango.

Serikali imetenga zaidi ya Sh1.9 bilioni kwaajili ya ujenzi huo.

Awali ofisi za Halmashauri hiyo zilikuwa eneo la KDC Manispaa ya Moshi ambapo zilihamishiwa eneo la Kolila na kusababisha watumishi na mwananchi kulazimika kupanda magari matatu kufika eneo zilizopo ofisi hizo.

Akizungumza leo Jumatano Agosti 25, 2021 wakati wa ziara yake katika eneo linalojengwa ofisi hizo mkuu  huyo wa mkoa, amesema serikali imeshatenga fedha za ujenzi hivyo kazi hiyo ianze haraka kupunguza kero za wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma.

 “Katibu Tawala (RAS)  wasiliana na Mkurugenzi kama kuna kitu kinachokwamisha na kuchelewesha kuanza ujenzi wa ofisi hapa tujue ili mtafute  namna ya kutatua lakini mpaka  Septemba 30 mwaka huu hizi  fedha ziwe  zimeshaanza kutumika kama Katibu Mkuu Tamisemi  alivyoelekeza,”amesema Kagaigai

 “ Hatuwezi kukwamisha maamuzi ambayo yamekwisha fanyika sitaki huu ujenzi uchelewe nikija hapa nikute ujenzi umeshaanza maana tayari serikali imeshatoa fedha kwa ajili ya kuanza kwa huu ujenzi,”amesema Kagaigai

Akizungumzia hatua ya ujenzi huo Msigala amesema michoro iko tayari na kubainisha kuwa hadi kukamilika kwa kazi hiyo itagharimu zaidi ya Sh2.9 bilioni.