Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

2,400 warudishwa kutoka Msumbiji

Muktasari:

Wakati Mhagama akieleza idadi ya Watanzania waliorudishwa nchini, mwanamke mmoja aliyekuwa akitokea  nchini Msumbiji amefariki dunia usiku wa kuamkia juzi katika Hospitali ya Rufaa Ligula mkoani Mtwara alikokuwa akipatiwa matibabu.

Mtwara. Ofisa wa Uhamiaji wa Mkoa wa Mtwara, Rose Mhagama alisema hadi sasa Watanzania 2,420 wamerudishwa nchini kutokea Msumbiji kupitia Mpaka wa Kilambo.
Mhagama alisema huenda idadi hiyo ikaongezeka kutokana na kuendelea kuwasili kwa wananchi hao.
Wakati Mhagama akieleza idadi ya Watanzania waliorudishwa nchini, mwanamke mmoja aliyekuwa akitokea  nchini Msumbiji amefariki dunia usiku wa kuamkia juzi katika Hospitali ya Rufaa Ligula mkoani Mtwara alikokuwa akipatiwa matibabu.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, George Salala alisema mwanamke huyo ametambuliwa kuwa ni Jackline Gryson (26) mkazi wa mkoani Iringa.
Alisema alipokewa katika kivuko cha mpaka wa Kilambo hali yake ikiwa mbaya kutokana na ugonjwa.
Wakati huohuo; Kaimu kamanda huyo alisema Mkoa wa Mtwara unaendelea kuwapokea Watanzania wanaorudishwa nchini kutokea Msumbiji wanakodaiwa kuishi kinyume cha sheria.