Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

2025 mwaka wa  uchaguzi wa wanawake kuonyesha uwezo

Mbunge viti maalum Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema ), Sophia Mwakagenda akiteta jambo na Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini, Dk Tulia Ackson mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ruanda nzovwe jijini hapa kwenye mashindano ya mapishi kwa baba na mama lishe. Picha na Hawa Mathias.

Muktasari:

  • Kauli hiyo imetolewa na Mbunge Viti Maalum, Sophia Mwakagenda leo Jumamosi Agosti 31, 2024,  akiwa miongoni mwa viongozi wa vyama vya siasa walioshiriki mashindano ya mapishi maarufu kama "Tulia cooking Festival 2024" katika viwanja vya Ruanda nzovwe jijini Mbeya.

Mbeya. Wakati Tanzania ikitarajia kufanya uchaguzi mkuu mwakani,  Mbunge Viti Maalum, Sophia Mwanagenda amewataka wanaume kujifungia ndani ili waonyeshwe uwezo wa  kuongoza kutoka kwa wanawake.

Mwakagenda  ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Agosti 31,2024 mara baada  ya kushiriki mashindano ya mapishi maarufu kama "Tulia Cooking Festival 2024" yaliyohusisha baba na mama lishe  1,000 yaliyofanyika  katika  viwanja vya Ruanda Nzovwe jijini hapa .

Kauli ya Mwakagenda iliibua shangwe kwa mamia ya wananchi walioshiriki wakiwemo viongozi wa CCM  wakiongozwa na  Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa NEC Mkoa  wa Mbeya , Ndele Mwaselela.

"Tunataka kuionyesha dunia kama wanawake tuna uwezo wa kuongoza nchi,  tunao viongozi   akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson  na Spika mstaafu, Anna Makinda ambao wamefanya vizuri katika kuliongoza Taifa," amesema Mwakagenda.

Amesema wakati wakielekea katika chaguzi zijazo umefika wakati wanaume wakae pembeni, wajifungie ili  wanawake waonyeshe uwezo wa kugombea nafasi za uongozi na kuliongoza Taifa na nchi kwa ujumla na sio familia pekee.

Amesema  miaka ya nyuma  walijulikana wana kazi ya kupika na sio kugombea  uongozi,   sasa wanataka kuonyesha  kama na wao wana uwezo wa kuongoza na kufanya vizuri.

"Tumeona hapa Dk Tulia ameandaa tukio hilo asilimia 90 ya wanawake wameshiriki, tunataka chaguzi zijazo mjitokeze kugombea ili kumuunga mkono "amesema Mwakagenda huku akishangiliwa.

Amesema licha ya kuwa mfuasi wa Chadema na kulala polisi,  lakini 4R za Rais Samis Suluhu Hassan zimewaweka vizuri.

Kwa upande wake,  Mwaselela amesema kama chama hawana muda wa kupoteza kumpa ridhaa  mtu mwingine kugombea   Mbeya mjini huku akimpongeza Mwakagenda kwa ushiriki wake katika mkusanyiko huo.

"Tutamlinda Dk Tulia Ackson kwa hali yoyote na kuhakikisha uchaguzi ujao anapata kura za kishindo ili aendelee kuwapigania wananchi wake kuleta maendeleo ya kweli kwa jimbo la Mbeya," amesema