Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Adaiwa kumshambulia mjamzito

Adaiwa kumshambulia mjamzito

Muktasari:

  • Mwenyekiti wa kijiji cha Samanga Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Wilfredy Minja anadaiwa kumshambulia na bakora Asha Rajabu (28) na kumsababishia maumivu huku polisi wakitangaza kuanza msako wa kumkamata mtuhumiwa.

Moshi. Mwenyekiti wa kijiji cha Samanga Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Wilfredy Minja anadaiwa kumshambulia na bakora Asha Rajabu (28) na kumsababishia maumivu huku polisi wakitangaza kuanza msako wa kumkamata mtuhumiwa.

Asha ambaye amelazwa katika hospitali ya Kilema inadaiwa alikuwa ni mjamzito ambao uliharibika kutokana na kipigo hicho kile kinachodaiwa cha mwenyekiti huyo, ambaye pia inadaiwa alikuwa na bastola na alifyatua risasi hewani

Kaimu Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Ronald Makona alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo, alisema binti huyo alishambuliwa kwa bakora na mtuhumiwa huyo sehemu za makalio na mapajani na kumsababishia maumivu makali mwilini.

“Ni kweli tukio hili lilitokea Januari 24 saa 6:00 usiku eneo la Marangu Maua ambapo mwenyekiti wa kijiji alimshambulia kwa kumchapa bakora sehemu mbalimbali za mwili na kumsababishia maumivu makali,” alisema.

Kuhusu mwenyekiti huyo kutumia silaha, Kamanda Makona alisema wanamchunguza kwani tukio hilo limefika ofisini kwake jana na upekuzi unaendelea.

“Jitihada za kumtafuta na kumkamata mtuhumiwa zinafanyika na chanzo cha tukio hilo bado tunachunguza, tayari nimeshatuma timu yangu kwenda Marangu ili kujua ni kweli alikuwa na silaha hiyo na tutampekua,” alisema

Mkuu wa wilaya ya Moshi, Rajabu Kundya alikiri kupokea taarifa za tukio hilo na kwamba, amelielekeza jeshi la polisi kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria.

“Nimewaelekeza polisi kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria ili kila anayehusika na tukio hilo achukuliwe hatua zinasostahili,” alisema na kuongeza

“Nimesikia kuna bastola ilitumika, hilo ni kosa na polisi wazuie silaha hiyo kwanza mpaka tujiridhishe kama ni halali na kama anaitumia inavyotakiwa, kisha mengine yatafuata,” alisema Kundya.