Adaiwa kumuua dada yake, kisa fedha za nyanya
Muktasari:
Mkazi wa kijiji cha Urauri ,kata ya Reha wilayani Rombo, Magreth Mushi ameuawa na kaka yake, Neoni Lazaro kwa madai ya kugombania fedha alizouza nyanya.
Rombo.Mkazi wa kijiji cha Urauri ,kata ya Reha wilayani Rombo, Magreth Mushi ameuawa na kaka yake,Neoni Lazaro kwa madai ya kugombania fedha alizouza nyanya.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Ronald Makona amesema tukio hilo limetokea Februari 9, mwaka huu.
"Februari 9,mwaka huu majira ya saa tatu katika kijiji cha Urauri Mwanamke aitwaye Magreth Mushi alijeruhiwa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na kaka yake ," amesema Kamanda Makona
Ameongeza "majeruhi alipopelekwa Hospitali ya Huruma kwa ajili ya kupatiwa matibabu alifariki dunia usiku huo wa kuamkia Februari 10 mwaka huu,"
Kamanda Makona amesema mwili wa mwanamke huyo umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti , Hospitali ya Huruma.