Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Addis Ababa yaandaa sheria kupiga marufuku malaya, ombaomba

Muktasari:

Hadi sasa sheria za nchi hiyo haijakataza biashara ya kuuza miili, lakini mapendekezo ya mpango huo yatalenga malaya wa mitaani na si kwenye baa, nyumnba za wageni na masaji

Viongozi nchini Ethiopia wanaandaa muswada wa marufuku biashara ya kuuza miili, maarufu kama umalaya, na ombaomba mitaani ikiwa ni kati ya hatua zinazolenga kusafisha taswira ya nchi, ofisi ya meya ilisema jana Alhamisi.
Muswada wa sheria unaoeleza masharti ya marufuku hiyo uko katika hatua za mwisho za maandalizi.
Lakini Feven Teshome, ofisa habari wa ofisi ya meya wa Addis Ababa ambao ni mji mkuu wa Ethiopia, aliiambia AFP kwamba kuna haja ya kukabiliana na hali ya "matatizo ya kijamii" inayozidi kuwa mbaya katika jiji hilo lenye watu zaidi ya milioni tatu.
"Tunakisia kuna zaidi ya ombaomba 50,000 na zaidi ya malaya 10,000 wa mitaani jijini Addis Ababa. Muswada wa sheria unalenga kuondoa matatizo haya ya kijamii ambayo yanatengeneza picha mbaya ya Ethiopia," alisema Feven.
Biashara ya kujiuza bado haijaharamishwa kisheria nchini Ethiopia, na Feven alisema mapendekezo ya kuipiga marufuku jijini Addis Ababa kutahusisha wale wanaosumbua watu mitaani.
Hii inamaanisha haitahusisha baa, maeneo ya kulamda miili, nyumba za wageni na mengine ambako umalaya umetamalaki.
Wauza miili na wateja wao wote watakabiliwa na adhabu ambazo zinaweza kuwa ni faini au kifungo.
Hali kadhalika, marufuku kwa ombaomba pia itahusisha wale wanaowapa fedha.
Mwezi Mei, viongozi wa Ethiopia walipitisha uamuzi wa kudhibiti unywaji pombe na uvutaji sigara katika maeneo ya wazi.
Hatua hiyo pia ilihusisha kupiga marufuku uuzaji wa pombe kwa yeyote aliye na umri chini ya miaka 21.
Katika kukabiliana na uvutaji sigara, katika siku za karibuni polisi wamevamia klabu za usiku walizohisi zinauza shisha au uvutaji sigara, na kuwaweka kizuizini kwa muda wateja na wafanyakazi wa maeneo hayo.