Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Alichokisema Frederick Sumaye kuhusu Lowassa kurejea CCM

Muktasari:

Waziri Mkuu mstaafu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Frederick Sumaye amesema uamuzi uliochukuliwa na Edward Lowassa kurejea CCM hauwezi kuwateteresha


Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye amesema uamuzi uliochukuliwa na Edward Lowassa kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM) hauwezi kumshtua.

Sumaye ambaye pia ni Waziri Mkuu mstaafu akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Machi 1, 2019 muda mfupi baada ya Lowassa kuchukua uamuzi huo amesema, “Mimi haunipi shida, mtu akiamua kuhama chama na kwenda kingine ni uamuzi wake.”

Akijibu swali la Mwananchi kama naye ni miongoni mwa watakaorejea, Sumaye amesema, “Kama kaamua acha aende, sisi tutaendelea kujenga chama na hicho unachokisema cha kuhama ni ndoto ambayo haipo.”

Lowassa aliyetangaza kuhama CCM Juni 28 mwaka 2015 baada ya kueleza kutoridhika na mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya chama hicho, leo Ijumaa ametangaza kurejea CCM na kupokelewa na Mwenyekiti wa chama hicho tawala nchini Tanzania, Rais John Magufuli.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi